Form 2 Kiswahili – UUNDAJI WA MANENO

Share this post on:

Uundaji wa maneno ni shughuli ya kuunganisha viambajengo (vipashio) mbalimbali ili kupata maneno tofauti yenye maana mbalimbali ambazo ni kamili.

Kwa kuwa maendeleo ya jamii hubadilika, hukua na kuongezeka hivyohivyo lugha nayo hukua na kubadilika kwa lengo la kukidhi haja ya mawasiliano.

Ili msamiati uongezeke lazima maneno yaundwe kwa lengo la kuboresha mawasiliano kulingana na wakati uliopo.

UMUHIMU WA UUNDAJI WA MANENO

  1. Kupata msamiati wa kutosha katika lugha husika ili kukidhi mabadiliko yanayojitokeza.
  2. Kukabiliana na suala la maendeleo ya sayansi na teknolojia katika ongezeko la maneno mapya.
  3. Ubunifu wa maneno mbalimbali hutokana na njia mbalimbali kama vile uambishaji wa maneno, kubadili mpangilio wa herufi kutohoa maneno ya lugha nyingine, kuambatanisha maneno, kufananisha sauti, umbo, mlio.

edu.uptymez.com

UUNDAJI WA MANENO KWA KUTUMIA MOFIMU=

(a)  MOFIMU

  1. Maana

edu.uptymez.com
  • Mofimu ni kipashio kidogo chenye maana ya kisanifu na kileskia, kipashio hicho kinaweza kuwa sehemu ya neno au neno zima.
  • Mofimu yenye maana ya kileskia aghalabu huwa na mofimu ambazo haziambatanishwi na kipashio kingine chochote.
  • Mofimu – Ni kipashio kidogo kabisaa cha kiisimu ambacho kina maana kisarufi au kileksika.

edu.uptymez.com

Mfano; Baba, Mungu, Fikiri, bora

  • Mofimu zenye maana ya kisarufi ni mofimu zinazoambatanishwa na mofimu nyingine katika uundaji wa maneno. Mofimu hizo huwa ni sehemu tu ya maneno yanayoambatanishwa katika mzizi wa neno mfano:

edu.uptymez.com

       –  M – toto

       –  Tu – ta- pi – ka

       –   U – som – i

Katika Kiswahili, mofimu inaangaliwa katika daraja la vipashio vya lugha. kipashio hiki hakiwezi kuvunjwavunjwa zaidi bila kupoteza maana.

Mfano:

  1. Mtoto (Watoto)

edu.uptymez.com

–      Hapa kuna mofimu mbili katika neno hili mofimu ya kwanza ni m – ambayo ni mofimu ya kisarufi inayoonesha idadi (umoja) na ”wa” katika wingi.

–      Mofimu ya pili ni toto ambayo ndio shina la neno hilo, kwa kutumia shina hili unaweza kupata maneno mengine kama vile utoto, vitoto, kitoto, kijitoto.

–      Mofimu shina (toto) ni mofimu ya kileskia yaani ni mofimu yenye maana kamili na ambayo yaweza kutumika kuundia maneno mengine katika lugha.

–      Mofimu (m-) katika “mtoto” ni mofimu ambayo maana yake hudhihirika kutokana na kujitegemeza katika mofimu ya kileskia. Bila kujiegemeza kwenye mzizi wa neno maana yake haiwezi kubainika.

AINA ZA MOFIMU

Kuna aina kuu mbili za mofimu

(i)   Mofimu huru (sahihi)

(ii)  Mofimu tegemezi

  1. MOFIMU HURU/ SAHIHI

edu.uptymez.com

Ni mofimu inayoweza kusimama peke yake na kuweza kutumiwa katika tungo bila kuwa na kiambishi chochote. Mofimu huru zina hadhi ya neno na zinaweza kuwa aina yoyote ya neno kama vile: –

–  Majina (nomino): juma, simba, baba, mama, dada, kaka

–   Viwakilishi: mimi, sisi, yeye, wao, ninyi

–  Vivumishi: safi, chafu, kile, refu

–  Vitenzi: Sali, tafiti, jibu

–  Viunganishi: na, hata, hadi

–  Vielezi: haraka , polepole, sana, mno

  1. MOFIMU TEGEMEZI

edu.uptymez.com

Ni mofimu zinazofungamana na mofimu nyingine na zinapotumika hutegemeana ili kueleza dhana iliyokusudiwa. Mofimu hizi zinapofungamana huunda neno. Mofimu zinazounda neno huweza kuwa mbili au zaidi kulingana na mchangamano wa dhana ulio katika neno linaloundwa

Mfano:

Mtoto    –   m- toto

Watacheza   –  wa – ta – chez – a

Anasoma  –  a – na – som –a

Mkulima   –  m – ku – lim –a

NAFSI

      Nafsi               katika       umoja                nafsi         katika      wingi

    (i)  mimi                              NI                    sisi                         TU

    (ii)   wewe                             U                    ninyi                        M

     (iii)  yeye                             A                     wao                         WA

 
 

Mfano:-

Neno “analima” lina mofimu nne (4) ambazo hufungamana na kujenga neno “analima” kila moja ya mofimu hizi isimamapo peke yake haina maana yoyote isipokuwa ina maana kisarufi ambayo humuwezesha mwanaisimu kuchambua maana ya mofimu hiyo.

            Analima – a – na- lim – a

 A – kiambishi awali kipatanishi cha nafsi ya III umoja

Na – kiambishi awali cha wakati uliopo

Lim – mzizi wa neno

A – kiambishi tamati

Dhima kuu ya mofimu ni kuongeza msamiati. Msamiati huo unaweza kuongezeka kwa kuunda neno zima. Pia msamiati unaweza kuundwa kwa shina moja kwa kuweza kuunda na kutoa maneno yenye maana mbalimbali.

Mfano:-

Neno “cheza” linaweza kuwa : mchezaji, mchezo, wanachezea, tulicheza, uchezeshaji, alimchezesha n.k.

Vilevile mofimu tegemezi zina dhima mbalimbali tofauti na uundaji wa msamiati. Baadhi ya dhima hizi ni kama vile,

  1. kudokeza nafsi
  2. kuonesha njeo (wakati)
  3. kuonesha/ kudokeza urejeshi
  4. kudokeza ukanushi
  5. kudokeza kauli mbalimbali

edu.uptymez.com

(b)  UUNDAJI WA MANENO KWA KUTUMIA UAMBISHAJI

(i)   Maana

–      Uambishaji ni kitendo cha kupachika kiambajengo (mofimu) cha neno kwenye mzizi wa neno ili kukamilisha muundo wa neno

VIAMBISHI

–  Viambishi vinavyowekwa kwenye mzizi wa neno na kukamilisha muundo wa neno hilo. Viambishi vinaweza kuambilishwa kabla au baada ya mzizi wa neno (kiambishi kinaweza kupachikwa mwanzoni na mwishoni mwa mzizi wa neno ).

                            AU

–  Viambishi ni mofimu muhimu sana katika uundaji wa maneno mapya kutokana na mzizi wa neno moja.
                          
                              AU
–  Viambishi ni mofimu zinazowekwa kwenye mzizi wa neno na kukamilisha muundo wa neno.

Kwa mfano neno:  ANAYEJIPIKIA

Viambishi awali (mwanzoni) vyake ni A – NA- YE – JI

Viambishi tamati ni –I – A – na mzizi wa neno hilo ni – PIK-

AINA ZA VIAMBISHI

(a) Viambishi awali

–   Hivi ni viambishi vinavyowekwa kabla ya mzizi wa neno navyo ni vitano

(ii)  Viambishi ngeli

Mfano:

M – tu  =   wa – tu

M – ti   =  mi – ti

M – zuri  =  wa – zuri

M – safi  =  wa – safi

(iii) Kipatanishi (kiambishi awali cha nafsi)

Hivi hujitokeza katika vitenzi na wakati fulani huitwa viambishi awali vya nafsi

Mfano: –               Umoja                                     Wingi

                        Ni – nalima                         tu – nalima (nafsi 1)

                        U – nalima                          m – nalima (nafsi 2)

                        A – nalima                          wa – nalima ( nafsi 3)

(iv) viambishi awali vya wakati (njeo)

Hivi huonesha wakati tendo limefanyika katika kitenzi

Mfano: analima

A – na- lima  (wakati uliopo)

A – li – lima   (wakati uliopita)

A – ta – lima  (wakati ujao)

(v)  Viambishi awali vya hali

Hivi huonesha hali mbalimbali katika kitenzi

Mfano: –

Hu – lima   (hali ya mazoea)

A – me – lima   (hali timilifu)

A-   nge – lima  ( hali ya masharti)

(vi)  viambishi awali vya rejeshi vya mtendaji wa jambo au tendo (kiima)

Hivi hutaja mtenda wa jambo

Ni – na- ji – kata

A – na – ye – sema

U – li – o – enea

(vii) Viambishi awali rejeshi vya mtendwa

Hivi hutaja mtendwa wa jambo

Mfano: –

Tuli – u – panda

Nina – i – soma

Ana – m – piga

Wana – ni – soma

 
 

(viii) Viambishi awali vikanushi na yakinifu

Hivi huwekwa katika kitenzi ili kukamilisha hali ya kukanusha, viambishi vya kukanusha katika lugha ya Kiswahili ni ha – hu – na – si

Mfano: –

U – naimba               hu – imbi

Ni – nacheza             si – chezi

A – naimba               ha- imbi

(b)  Viambishi kati

Ni viambishi vinavyopachikwa ndani ya mzizi wa neno na hivyo kuukuta katika sehemu mbili. Viambishi kati havitokei katika Kiswahili lakini vipo katika sehemu nyingine, mfano kiebrania.

(c)  Viambishi tamati

Hivi ni viambishi vinavyoambishwa baada ya mzizi wa neno navyo ni vya aina mbili.

(i)    Viambishi tamati maana

Hivi hutokea baada ya mzizi wa kitenzi bila kubadilisha umbo la mzizi wenyewe. Viambishi tamati maana hutaja maana au dhana.

Mfano: –

Lim –a

Lim – wa

Chez – a

Chez – wa

(ii)  Viambishi tamati vijenzi

Hivi ni viambishi vinavyoandikwa baada ya mzizi wa kitenzi viambishi tamati vijenzi navyo hutokea mara baada ya mzizi wa kitenzi na vina kazi kuu nne.

(a)  Kuleta maana ya ziada ya kule kwenye maana ya asili iliyobebwa na mzizi wa kitenzi.

Mfano: –

Lima – limia- limika – limisha – limiwa

Tendo – tendea – tendeka – tendesha – tendewa

(b)  Kujenga mzizi mpya wa kitenzi ambao utabebeshwa maana ya asili ya kitenzi na maana ya ziada. Mzizi huu mpya huitwa “mzizi wa mnyambuliko”

Mfano: –

 
 

Kitenzi

 
 

Mzizi asilia

 
 

Mnyambuliko

 
 

Mzizi wa mnyambuliko

 
 

Piga

 
 

Pig –

 
 

Pigana

 
 

Pigan

 
 

Cheza

 
 

Chez –

 
 

Chezeka

 
 

Chezek

 
 

Imba

 
 

Imb –

 
 

Imbisha

 
 

Imbish

 
 

Ruka

 
 

Ruk –

 
 

Rukiana

 
 

Rukian

 
 

Lima

 
 

Lim –

 
 

Limika

 
 

limik

edu.uptymez.com

 
 

(d)  Huweza kubadili neno toka aina moja na kuingia aina nyingine

Mfano: –

Omba – ombeana – ombaji – ombeka – ombi – ombeaji          

  T              T          N            T           N          T

(e)  Kuweza kuzalisha kauli mbalimbali za tendo kama ifuatavyo;-                              

Kauli ya kutenda;-        Chez – a
                                   Chek – a

                                   Imb – a

Kauli ya kutendwa;-      Chez – wa

                                   Chek – wa

                                   Imb – wa

Kauli ya kutendeka;-      Chez – ek – a

                                   Chek – ek – a

                                   Imb – ik – a

Kauli ya kutendewa;-      Chez – ew –a

                                   Chek – ew – a

                                   Imb – iw – a

Kauli ya kutendea           Chez –e –a

                                    Chek – e – a

                                    Imb –i –a

Kauli ya kutendeana       Cheze – an – a

                                   Cheke – an – a

                                   Imbi – an – a

Kauli ya kutendesha       Cheze – sh – a

                                   Cheke – sh – a

                                   Imbi – sh – a

(a)  MZIZI KIINI CHA KITENZI

Mzizi au kiini ni ile sehemu ya neno inayobakia baada ya kuondolewa aina zote za viambishi yaani viambishi awali na tamati (mzizi ni sehemu isiyobadilika).

Kuna aina mbili za mzizi

(i)    Mzizi asilia

Huu ni mzizi unaobakia baada ya kuondolewa viambishi tamati vijenzi. Mzizi huu mpya hubeba maana ya ziada ya hivyo viambishi maana kama vile:

                       NENO                                                MZIZI ASILIA

                          Lima                                                 lim-

                         Lewa                                                 lew-

                         Cheza                                               chez-

                         Ona                                                   on-

(ii) Mzizi mnyambuliko

          Huu ni aina ya mzizi ambao hujengwa na mzizi asilia pamoja na viambishi tamati vijenzi. Mzizi huu mpya hubeba maana ya ziada ya hivyo viambishi.

Kitenzi           Mzizi asilia               Mnyambuliko          Mzizi mnyambuliko

Tema              tem                          Temana                      Teman

Pata                Pat                            Patisha                      Patish

Lia                   Li                              Lilika                          Lilik

Kula                Kul                            Liwa                           Liw

Soma              Som                          Somana                      Soman

(b)  SHINA LA KITENZI

Shina la kitenzi ni mzizi wowote (yaani mzizi asilia au mzizi wa mnyambuliko) uliofunguliwa irabu -a- isiyo na maana maalum ya sarufi.

Mzizi                         shina

Lim + a                      lima

Chez + a                   cheza

Fik +a                       fika

Liw +a                       liwa

Vitenzi vyenye asili ya kigeni ambao huishia na irabu e, i, u katika mzizi asilia yao.

Mfano: –

–  “arifu”

–  “tafiti”

–  “samehe”

–  “Sali”

–  “jibu”

Vitenzi hivyo, mzizi asilia na shina huwa kitu kimoja

Mzizi = shina + a

Shina  = mzizi + a

KUBAINISHA MOFIMU AU VIAMBISHI

Kubainisha mofimu (viambishi) ni kitendo cha kutenga neno katika mofimu au viambishi vinavyolijenga.

HATUA MUHIMU KATIKA KUBAINISHA MOFIMU

Hatua zifuatazo ni muhimu katika kubainisha mofimu nazo ni: –

(a)  Kutambua aina ya neno ( neno huru au changamano) huundwa na mofimu tegemezi. Neno huru halivunjwivunjwi lakini neno changamano linavunjwavunjwa na kubainisha mofimu zake. Mfano wa neno huru  =  dada, kaka, mama.

Mfano wa neno changamano  =   a – na – on – a

                                           =   anaona

(b)  Kutenga (kuvunjavunja) mofimu au viambishi vinavyounda neno hilo yaani tambua viambishi awali, mzizi, kiini na viambishi tamati. Viambishi na mzizi hupatikana katika neno changamano

Mfano: –

Bainisha mofimu katika maneno yafuatayo na eleza kazi za kila mofimu.

(i) Anasoma  –     a – na- som – a

                         1     2     3     4

  1. Kiambishi awali kipatanishi nafsi III umoja
  2. Kiambishi awali cha wakati uliopo
  3. Mzizi wa kitenzi
  4. Kiambishi tamati

edu.uptymez.com

(ii) Dunia  –    hili ni neno huru ambalo huundwa na mofimu hizi hazivunjwivunjwi

(iii) Waliompiga  –  wa – li- o – m – pig – a

                             1       2   3   4     5     6

  1. Kiambishi awali kipatanishi nafsi ya tatu wingi
  2. Kiambishi awali cha wakati uliopita
  3. Kiambishi awali rejeshi cha watenda
  4. Kiambishi awali rejeshi cha watendwa
  5. Mzizi wa kitenzi
  6. Kiambishi tamati

edu.uptymez.com

DHIMA YA MOFIMU/ VIAMBISHI

  1. Kuonesha nafsi katika kitenzi

edu.uptymez.com

Mfano: –

Ni – nasoma= Tu – nasoma  – I

U – nasoma   =  m – nasoma   – II

A – nasoma   =  wa – nasoma- III

  1. Kuonesha njeo katika vitenzi

edu.uptymez.com

Mfano: –

A – na – cheza   –   wakati uliopo

A – li – cheza   –    wakati uliopita

A – ta – cheza –    wakati ujao

  1. Kuonesha umoja na wingi katika nomino na viambishi

edu.uptymez.com

Mfano: –

M – toto =  wa – toto

Ki – su  =   vi -su

  1. Kuonesha hali mbalimbali za kitenzi

edu.uptymez.com

Mfano: – hali ya masharti

A – ki – ja

A – nge – ku – ja

–  Hali ya kuendelea kwa tendo = a – na – li – ma

–  Hali timilifu=  a – me – sem – a

–  Hali ya mazoea=  hu – soma                                                                    

  1. Kuonesha uyakinishi na ukanushi katika vitenzi

edu.uptymez.com

Mfano: –   ni – nalima   –   si – limi

              A – nacheza  –   ha – chezi

               U – naimba   –  hu – imbi

  1. Kuonesha urejeshi wa mtenda au mtendwa katika kitenzi

edu.uptymez.com

Mfano: –   A – na – ye – lima    –   Mtenda

              A – na – u – penda   –   mtendwa

  1. Kuonesha kauli mbalimbali za vitenzi

edu.uptymez.com

Kauli ya kutenda      – a – na – pik – a

Kauli ya kutendea    – a – na -pik -i – a

Kauli ya kutendewa-   a – na – pik – iw – a

Kauli ya kutendeana   – wa – na – pik – ian – a

Kauli ya kutendesha    –  a – na – pik – ish – a

Kauli ya kutendwa   –   a – na – pik – w – a

TOFAUTI YA MOFIMU NA SILABI

 
 

NA

 
 

MOFIMU

 
 

SILABI

 
 

1

 
 

Mofimu ni kipashio cha kiima chenye maana kisarufi na kileksia kamusi

 
 

Ni sehemu ya neno ambayo huweza kutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu la sauti

  

 
 

Kila mofimu ina kazi maalum kisarufi

(mfano) analima

A – na – lim – a

 
 

Si kila silabi ina kazi maalumu mfano silabi ”bali” ikisimama peke yake haiwakilishi maana yoyote kisarufi

  

  

 
 

Katika mofimu kuna viambishi awali na tamati

 
 

Katika silabi hakuna viambishi hivyo

  

  

 
 

Katika mofimu kuna mizizi, shina la neno

 
 

Katika silabi hakuna mzizi wala shina.

  

 
 

Mofimu huru hazivunjwivunjwi, hubaki zilivyo mfano; neno baba lina mofimu huru moja

 
 

Silabi huvunjavunja hata mofimu huru mfano;

baba – ba + ba = silabi mbili

  

 
 

Mofimu hazivunjivunji mzizi wa neno mfano;

Lima mzizi lim

 
 

Silabi huvunjavunja mzizi wa neno mfano; “analima” lina silabi nne

A –   na – li – ma

1     2       3     4

  

 
 

Mara nyingi katika neno kuna idadi ndogo ya mofimu. Mfano; “mama” lina mofimu moja, anacheza lina mofimu nne

 
 

Mara nyingi katika neno kuna idadi nyingi za silabi. Mfano;

Mama – lina silabi mbili

Anacheza – lina silabi nne

edu.uptymez.com

 
 

(c)  UUNDAJI WA MANENO KWA KUTUMIA MNYAMBULIKO

Unyambulishaji unatokana na neno “nyambua” ikiwa na maana refusha au vuta kitu.

         Mnyambuliko ni kitendo cha uvutaji au urefushaji kipashio / vipashio katika mzizi wa neno. Aidha mnyambuliko unahusu upachikaji wa mofimu zinazofuata mzizi wa neno. Mofimu hizi huitwa mofimu fuatishi (viambishi tamati)

Mfano:-

Soma –  Som – e – a

             Som – ek –a

             Som – esh – a

             Som – w – a

             Som – ean – a

              Som – o

Vitenzi

Vitenzi vyote vya Kiswahili isipokuwa kitenzi kishirikishi “ni” vinaweza kunyambulika.

Mfano: –

Piga – pigia, pigana, pigisha, pigwa, pigiana, cheza, chezea, chezeana, chezeshwa, chezwa.

Baadhi ya majina ya ujumla hupokea viambishi tamati na mengine hupokea viambishi tamati vijenzi.

Mfano: –

Nyumba  –   nyumbani

Bustani   –   bustanini

Hewa     –   hewani

Maji       –   majini

Viwakilishi

Hivi huchukua viambishi tamati maana

Mfano: –

(a)  Viwakilishi vya nafsi kama vile

Mimi     –  miye

Wewe   –  weye

Sisi       – siye

Ninyi    –  niye   

(b)  Viwakilishi virejeshi vya amba.

–   Ambalo

–   Ambacho

–   Ambavyo

Vivumishi

Hivi huchukua viambishi tamati vijenzi

Mfano: –        

Safi     –   safisha, safishwa, safishia, safishika

Fupi    –  fupika, fupisha, fupishika, fupishwa

Refu    –   refusha, refushwa, refushika

Viunganishi

Hesabu ndogo ya viunganishi huchukua viambishi tamati vitenzi.

Mfano : – Labda, labdatisha, labdilika, labdishwa.

DHIMA YA MNYAMBULIKO

(i)   Mnyambuliko wa maneno hukuza msamiati wa lugha husika.

(ii)   Mnyambuliko wa maneno hupanua maana ya maneno.

(iii)  Mnyambuliko wa maneno huzalisha kauli mbalimbali za vitenzi kutenda, kutendwa, kutendea, kutendeka, kutendana, kutendeana kutendesha, kutendeshwa.

 

 
 

Share this post on: