Form 3 Kiswahili – MJENGO WA TUNGO

Share this post on:

Tungo – Ni neno au maneno yanayotoa taarifa fulani ambayo yanaweza kuwa kamili au yasiwe kamili.

Neno hili tungo ni nomino ambayo hutokana na kitenzi ‘tunga’ ambacho kinamaana ya kushikanisha vitu pamoja kwa kupitisha kitu mfano uzi kwenye sindano.

Kisintaksia

Neno tungo humaanisha kupanga pamoja vipashio sahihi ili kujenga vipashio vikubwa zaidi. Katika lugha, tungo ya chini kabisa ni neno ambalo linaundwa na mofimu na tungo ya juu kabisa ni sentensi.

AINA ZA TUNGO

Kuna aina kuu 3 za tungo nazo ni;

  1. Tungo kirai
  2. Tungo kishazi
  3. Tungo sentensi

edu.uptymez.com

TUNGO KIRAI (KIKUNDI)

KIRAI
– Ni tungo isiyo na muundo wa kiima na kiarifu au ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja na kuendelea lakini ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu.

AU

Ni kipashio ambacho sio lazima kiwe na kitenzi

Kwa kawaida kirai ni kikubwa kuliko neno lakini ni kidogo zaidi ya kishazi

Katika kiwango hiki miundo ya tungo huhusisha maneno mawili au zaidi ambayo huwekwa pamoja katika mpangilio maalamu unaozingatia uhusiano uliopo baina ya neno kuu na maneno mengine.

AINA ZA VIRAI

  • Kirai Nomino (KN)

edu.uptymez.com

Ni kirai kinachotawaliwa na nomino au mahusiano ya nomino na neno au mafungu ya maneno

Muundo wa Kirai Nomino ni kama ifuatavyo

  • Nomino peke yake

edu.uptymez.com

Mfano;   Baba analima.   Juma anasoma

  • Nomino mbili au zaidi zinazounganishwa

edu.uptymez.com

Mfano; Juma na Ali wanacheza mpira.   Kaka na dada wanaenda sokoni

  • Nomino na kivumishi (N + V)

edu.uptymez.com

Mfano; Mwalimu hodari ameandaa somo. Mtoto mzuri anacheza

  • Kivumishii na nomino (V + N)

edu.uptymez.com

Mfano; Wale wazee wameondoka

  • Kiwakilishi peke yake

edu.uptymez.com

Mfano; Mimi ninasoma kitabu. Wewe unaumwa malaria

  • Nomino na kitenzi jina

edu.uptymez.com

Mfano; Kilimo cha kufa na kupona kimezingatiwa.   Kucheka kwa fisi hakunitishi

  • Kirai Kitenzi (KT)

edu.uptymez.com

Ni kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi au katika uhusiano wa kitenzi na neno au mafungu mengine ya maneno. Kirai kitenzi kimeundwa na vipashio vifuatavyo;-

  • Kitenzi peke yake (T)

edu.uptymez.com

Mfano; analima, anapika

  • Kitenzi + jina na kielezi

edu.uptymez.com

Mfano; Anamfundisha mtoto vizuri.   Wanasoma kivivu

  • Kitenzi kisaidizi kimoja au zaidi na kitenzi kikuu (Ts + Ts + T/Ts + T)

edu.uptymez.com

Mfano; Alikuwa analima.   Alikuwa anataka kulala

  • Kitenzi kishirikishi + Nomino (shamirisho)

edu.uptymez.com

Mfano; Ni mpole.   Ndiye shujaa

  • Kirai Kielezi (KE)

edu.uptymez.com

Miundo yake hailekei kukitwa kwenye mahusiano baina ya neno kuu (kielezi) na neno au fungu la maneno linaloandamana nacho. Badala yake miundo inayohusika hapa ni ya maneno ambayo hufanya kazi pamoja katika lugha.

Mfano; Wanafunzi wanaandika vizuri.   Alitembea polepole sana

Kazi kubwa ya miundo hii katika sentensi ni kueleza wakati, mahali, jinsi na kinachofanya tendo lifanyike. Tofauti na virai vingine ambavyo nafasi yake ndani ya sentensi huwa ni ya kudumu. Virai vielezi huweza kushika nafasi mwanzoni mwa sentensi au baada ya kitenzi.

Mfano; Juma alikuja jana jioni.   Jana jioni, Juma alikuja

  • Kirai Kihisishi (KH)

edu.uptymez.com

Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina vihisishi hivi; kwa, na, katika, au na fungu la maneno linaloandamana nalo. Katika kirai kihusishi neno kuu ni kihisishi katika Kiswahili, muundo wa KH ni mmoja tu, nao ni kihisishi na kikundi nomino

Mfano; Kwa amri ya jeshi. Mwizi amekamatwa na polisi. Amekwenda kwa kaka yake

TUNGO KISHAZI

Kishazi ni tungo yenye kitenzi. Kitenzi hicho kinaweza kuwa kinachojitosheleza na hapo huitwa kishazi huru au kikuu au chaweza kuwa kitenzi kinachojitegemea na hivyo huitwa kishazi tegemezi

AU

Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho kinaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kutegemea kingine

AINA ZA VISHAZI

Kuna aina mbili za vishazi

(i ) Vishazi  huru

(ii) Vishazi  tegemezi

Vishazi huru

Ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kikuu ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe uliokamilika usiohitaji maelezo zaidi ya kukamilisha maana.

Pia maana kamili yaweza kupatikana hata kama vishazi tegemezi vikifutwa katika sentensi zinazohusika, juu ya hayo vishazi huru vyaweza kuwa kabla au baada ya vishazi tegemezi

Mfano; watoto wazuri wanakimbia

Mama anapika chakula

Asha naye mpumbavu

Vishazi Tegemezi

Ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kisaidizi ambacho kwa tabia yake hakikamilishi ujumbe uliokusudiwa bali hutegemea kitenzi kikuu kuweza kutoa ujumbe uliokusudiwa

Mfano; mzee aliyekuja jana

Mbwa aliyepata kichaa

Nyumbu aliyepigwa risasi

SIFA ZA VISHAZI TEGEMEZI

  • Kishazi tegemezi hakitoi maana kamili ikiwa hakijaambatana na vishazi huru. Mfano; Somo lililoanza asubuhi. Mtoto aliyekuja jana
  • Vishazi tegemezi vinaweza kufutwa katika sentensi bila ya kuharibu maana kamili ya sentensi nzima. Mfano;   mtoto aliyekuja jana amekwenda sokoni. Katika sentensi hii kishazi tegemezi ‘aliyekuja jana’ kinaweza kufutwa na kupata sentesi kama; Mtoto amekwenda sokoni
  • Vishazi tegemezi aghalabu vinaweza kutambulika kwa kuwa na viambishi rejeshi. Mfano; aliyekuja Jana ameondoka. Kitabu kilichopotea juzi kimeonekana
  • Vishazi tegemezi vinaweza kutambulika kwa kuwepo vishazi tegemezi kama vile; kwamba, ingawa, ili, kwasababu, mpaka na vinakitwa hivi kwa ajili ya vihisishi vilivyopo. Mfano; a) Hamisi anasema kwamba watoto wengi wamekuwa wahuni, b) tumeingia shuleni ili tupate elimu.
  • Vishazi tegemezi vinaweza kutanguliwa au vikafuatiwa na vishazi huru. Mfano; i) nilimuona Rehema nilipokwenda sokoni, ii) utakuja nyumbani leo, kufuatana na ndugu yako.

edu.uptymez.com

AINA ZA VISHAZI TEGEMEZI

Vishazi tegemezi vinaweza vikawa na tungo kama hizi

  1. Tungo zenye viambishi rejeshi vya viwakilishi nafsi au viambishi ngeli vilivyoambatanishwa ndani ya kitenzi au mwisho.

edu.uptymez.com
  • Anayevunja sheria lazima aadhibiwe haraka
  • Kilichopotea sikijui
  • Miti iliyoanguka imeibiwa pande hizi

edu.uptymez.com

Vishazi kama hivi vilivyoelezwa hapo juu huwa vishazi tegemezi vivumishi (v) kama inavyoonekana kuna vishazi vilivyotumiwa pamoja na jina lake linalovumishwa.

  1. Tungo zenye kueleza mahali wakati masharti au kasoro na sababu. Vishazi tegemezi vielezi (E), mfano

edu.uptymez.com
  • Ninamolala mna kunguni wengi
  • Alipoondoka walifika wageni
  • Ukija nitakupa hicho kitu
  • Japokuwa inanyesha mvua nitatoka nje hivi punde

edu.uptymez.com
  1. Vishazi vyenye vitenzi vinavyoanza na kiambishi Ku – vilivyoambatana na maneno mengine. Mfano;

edu.uptymez.com
  • Saidi hataki kununua matunda sokoni
  • Kukaa tu, akatokea mjomba wangu
  • Kuulizwa tu, wakataka kuondoka

edu.uptymez.com

DHIMA NA HADHI YA VISHAZI

Kishazi huru kina hadhi ya sentensi (sentensi sahihi) lakini kishazi tegemezi hakina hadhi hii. Vishazi tegemezi ambavyo hutegemezwa kwenye vishazi vingine katika tungo ambavyo huwa kwa kawaida ni dhima ya kikundi au neno. Vishazi hivyo huvumisha nomino iliyoko kwenye tungo hiyo. Mfano;

(a) Askari walioenda vitani wamepewa mshahara

(b) Shule iliyofunguliwa kijijini imepata walimu

Vishazi tegemezi vingine hufanya kazi ya vielezi viwapo katika tungo, sawa na vikundi vielezi kutokana na hali hii, vishazii huru navyo huwa pia vimehusishwa hadhi, kwani vimeteremka daraja kutoka kishazi na kuwa sawa na kikundi ambacho kwa kawaida kina hadhi ndogo kuliko kishazi . mfano; (a) Juma alipigwa, alipoiba mahindi. (b) watoto walikimbia alipowaona

KIKUNDI SENTENSI

Sentensi

Ni kifungu cha maneno  kuanzia neno moja na kuendelea chenye kiima na kiarifu na kinaleta maana kamili. Sentensi ndio kipashio cha juu kabisa katika daraja la vipashio vya lugha

Muundo wa sentensi una sehemu kuu mbili yaani kiima na kiarifu (kikazi/kidhima) ina KN na KT (kimuundo)

KIIMA – ni sehemu au nafasi inayokaliwa na nomino au kikundi nomino ambacho kinaweza kujulikana mara nyingi kuwa mtenda

Mfano; Ali/ amewapiga watoto

Yeye/ ananitukana

Mkulima na bwana shamba/ wamelima kwa pamoja

KIIMA

Kiima ni sehemu au nafasi katika sentensi inayokaliwa na jina au kikundi jina ambacho huwa na kiambishi awali kipatanishi katika kitenzi kikuu. Mfano; Juma analima

Vipashio vya kiima

Kiima huundwa na;

  • Jina (N) mfano; Mtoto/ anacheza mpira
  • Jina na jina (N + N); Baba na mama? Wanalima
  • Jina + kishazi tegemezi kivumishi (N + V); Kitu kinachompendeza/ ni kuwa na nguo nzuri
  • Kivumishi na jina (V + N); Yule mtoto/ ni mzuri
  • Kiwakilishi peke yake; Wewe/ huna matatizo
  • Kitenzi jina: kilimo cha kufa na kupona/kinaanzishwa nchini. Kuimba na kucheza/ kwako/kunafurahisha. Kuiba/ hakupendezi
  • Jina + kivumishi. Watoto wote/ni watundu

edu.uptymez.com

KIARIFU

Ni sehemu inayokaliwa na maneno yanayoarifu funzo lililofanywa, linalofanywa au litakalofanywa.

AU

Ni sehemu au nafasi inayokaliwa na kishirikishi peke yake au kitenzi kikuu kimetumika sambamba na kitenzi kisaidizi kimoja au zaidi.

Mfano; Kaka alikuwa anaumwa

Vipashio vya kiarifu

  • Kitenzi kikuu – Haji/ atalima kesho asubuhi. Karama/ anacheza mpira
  • Kitenzi au vitenzi visaidizi vinavyoambatana na kitenzi kikuu

edu.uptymez.com

Mfano, mtoto/ alikuwa analima kila mara

Wavulana/ walikuwa wamekwisha kula

  • Kitenzi kishirikishi na nomino

edu.uptymez.com

Juma ni mtoto

Mtoto/ ni mgonjwa

SHAMIRISHO

Ni sehemu au nafasi inayokaliwa na nomino au kikundi nomino ambacho kinaweza kujulikana kuwa ni mtendwa, mtendewa au kitendwa (a/a)

Mfano; (a) Juma amempiga mtoto,

                             Mtendwa(sh)

(b) Mwalimu amempa mtoto zawadi

                               (mtendewa)

(c) Mwalimu amempiga mtoto fimbo (a/a)
                                (mtendwa)

CHAGIZO

Ni sehemu au nafasi inayokaliwa na kiulizi au kikundi kielezi. Chagizo huweza kutokea mara baada ya kitenzi kikuu au shamirisho

Mfano; Juma ataondoka kesho

   Mama   anasoma     kitabu     polepole

     N           T               Sh       Ch

AINA ZA SENTENSI

1. Sentensi sahili. Hii ni sentensi ya kishazi huru, kishazi hiko kinaweza kuwa na kifungu kitenzi kimoja, kifungu kitenzi hicho kinaweza kuwa cha kitenzi kikuu, kisaidizi au kishirikishi

Mfano;

  • Ali analima shamba

edu.uptymez.com

           T

  • Musa ni mzembe

edu.uptymez.com

                         t    

  • Mzee alikuwa  anataka  kwenda  kuona mpira

edu.uptymez.com

                        Ts           Ts         Ts

Sifa za sentensi sahili

  • Ina kiima ambacho kimetajwa wazi, kiima hicho huweza kuwa jina, jina na jina au jina na kivumishi
  • Ina kiarifu ambacho kimeundwa na kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kishirikishi au kitenzi kikuu  na kisaidizi pamoja na shamirisho na chagizo
  • Haifungani na sentensi nyingine na hivi inajitosheleza kimuundo na kimaana

edu.uptymez.com

2. sentensi changamano. Hii ni sentensi inayoundwa na kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi

Mfano; Nyumbu aliyepigwa risasi amekufa

Miundo ya sentensi changamano

  • Muundo wenye kishazi tegemezi vumishi
  • Mtoto anayeumwa kichwa amepona
  • Kisu kilichopotea juzi kimepatikana leo asubuhi
  • Muundo wenye kishazi tegemezi kielezi
  • Juma alikimbia aliponiona
  • Saidi hataki kununua matunda sokoni

edu.uptymez.com

3. Sentensi ambatano. Hii ni sentensi ambayo huundwa na sentensi mbili au zaidi  ambazo huunganishwa kwa kiunganishi. Miundo ya sentensi ambatano ni;

  • Muundo wa sentensi sahili (vishazi huru) viwili au zaidi vilivyoambatanishwa kwa kutumia viunganishi
  • Mama analima na baba anapanda
  • Yeye anapenda kusoma na mwanawe anapenda kucheza
  • Juma ni mrefu lakini saidi ni mfupi
  • Sentensi sahili (kishazi huru) pamoja na tungo changamano
  • Mtoto aliyekuja jana amekwenda sokoni lakini mama yake anapika jikoni
  • Msichana uliyemwona juzi ameondoka na mimi nimefurahi ameondoka salama
  • Muundo wenye sentensi changamano mbili zilizounganishwa kwa kiunganishi
  • Ng’ombe aliyezaa amepotea na ndama aliyezaliwa amekufa
  • Mtoto aliyesimama njiani ni mwanangu lakini yule aliyekaa chini ni mwanafunzi
  • Miundo yenye vishazi visivyo unganishwa kwa viunganishi, Vishazi vyote vinavyohusika katika miundo ya aina hii ina virai vitenzi vyenye kiambishi tamati – e na hiki kinaeleza hali ya matibabu au nia ya kutenda jambo. Kila kishazi katika miundo kama hii kikiendelezwa katika muktadha wa sentensi kubwa kinakuwa sentensi inayojitegemea
  • Niambie, niondoke
  • Mwache, aende tu
  • Mfundishe, aelewe

edu.uptymez.com

4. Sentensi shurutia. Hii ni sentensi ambayo ina vishazi tegemezi viwili ambavyo hutegemezi wake hutokana na mofimu – nge – ngali – ngeli – ki

  • Angejibu maswali angefaulu mtihani
  • Juma angelikuja mapema angelimkuta Mussa

edu.uptymez.com

UCHANGANUZI WA SENTENSI

Kuchanganua sentensi ni mbinu ya kuigawa sentensi katika sehemu mbalimbali ambazo huunda sentensi hiyo

Hatua za uchanganuzi wa sentensi

  • Kutaja aina ya sentensi yaani kama ni sentensi sahili, ambatano au changamano.
  • Taja sehemu zake kuu yaani; kiima na kiarifu (kishazi) au KN na KT (kimuundo)
  • Kama ni sentensi sahili onyesha vipashio vya kiima na kiarifu; yaani jina, vivumishi, vitenzi, shamirisho na chagizo n.k

edu.uptymez.com

Kama ni sentensi changamano taja vishazi vyake na kazi ya kila kishazi tegemezi katika hiyo sentensi changamano yaani taja: kama kishazi tegemezi kinavyovumisha jina au KN kilicho katika kiima au KN cha kishazi huru. Mfano; Mzee uliyemwona jana ni baba yangu. “uliyemwona jana” ni kishazi tegemezi kivumishi kinachovumisha jina “mzee” lililo kiima cha kishazi huru (K/H) “mzee ni baba yangu”

  • Kutaja aina za maneno yote yaliyomo katika sentensi hiyo. Mfano;

edu.uptymez.com

Baba na mama wanakula ugali

        N       t      N         T      N

  • Kuandika tena sentensi

edu.uptymez.com

NJIA YA UCHANGANUZI WA SENTENSI

Kuna njia kuu nne za uchanganuzi wa sentensi

  • Matawi/ ngawe/ michoroti
  • Jedwali/ visanduku
  • Mishale/ mistari
  • Sentensi/ maelezo/ maneno

edu.uptymez.com

Mfano;

  • Mwalimu mwema amemsaidia mwanafunzi

edu.uptymez.com

edu.uptymez.com

Mwalimu mwema amemsaidia mwanafunzi

  • Mbuzi aliyenunuliwa juzi amechinjwa leo asubuhi

edu.uptymez.com

 edu.uptymez.com

                 Mbuzi     aliyenunuliwa juzi amechinjwa leo asubuhi

VISANDUKU/ JEDWALI            

Mfano;

  • Gari lililopinduka jana limeinuliwana dereva wake amefariki dunia

edu.uptymez.com

S. ambatano

S1

  

S2

K

  

A

U

 
 

U

 
 

na

  

K

A

  

  

KE

KT

  

  

KT                         KN

N

V

E

T

N

V

T                             N

 
 

Gari

  

 
 

lililopinduka

  

 
 

jana

  

 
 

limeinuliwa

  

 
 

dereva

 
 

  

 
 

wake

 
 

  

 
 

Amefariki             dunia                        

  

edu.uptymez.com

 
 

 
 

  • Wanafunzi waliimba wimbo wao vizuri sana

edu.uptymez.com

 
 

                                                                   S. Sahili

         K

                                         A

KN        

             KT

               KN

                 KE

N

               T

     N

     V

                   E

Wanafunzi

waliimba

wimbo

wao

Vizuri sana

edu.uptymez.com

 
 

MISHALE/ MISTARI

Mfano;

  • Shangazi anasoma kitabu polepole

edu.uptymez.com

edu.uptymez.com

 
 

  • Mbwa aliyepata kichaa mwogope

edu.uptymez.com

edu.uptymez.com

MANENO/ MAELEZO

  • Juma anacheza mpira na Damasi anasoma kitabu

edu.uptymez.com

Hii ni sentensi ambatano

Sentensi hii ina sentensi mbili na kiunganishi

Sentensi ya kwanza ina kiima na kiarifu

Kiima kina jina

Jina ni juma

Kiarifu kina kitenzi na nomino

Kitenzi ni anacheza

Nomino ni mpira

Kiunganishi ni na

Sentensi ya pili ina kiima na kiarifu

Kiima kina jina

Jina ni Damasi

Kiarifu kina kitenzi na jina

Kitenzi ni anasoma

Jina ni kitabu

  • Balozi wetu ni mtu jasiri sana

edu.uptymez.com

           Hii ni sentensi sahili

           Sentensi ina kiima na kiarifu

           Kiima kina jina na kivumishi

           Jina ni balozi na kivumishi ni wetu

           Kiarifu kinakitenzi kishirikishi + Kirai nomino

           Kirai kielezi

           Kitenzi kishirikishi ni Ni

           Kirai nomino kina jina na kivumishi

           Jina ni mtu na kivumishi ni sana

 

Share this post on: