Form 3 Kiswahili – VITABU TEULE VYA FASIHI

Share this post on:

UCHAMBUZI WA RIWAYA.

Jina la kitabu: TAKADINI

Mwandishi: BEN J. HENSON

Wachapishaji: METHEWS BOOKSTORE AND STATIONERS

Mwaka: 2004

A: UTANGULIZI

Takadini ni riwaya inayoeleza maisha ya jamii za Kiafrika na tamaduni zao. Hii ni desturi ambayo imeandikwa kulenga watu au jamiii ya watu wanaokumbatia mila na desturi zilizopitwa na wakati. Riwaya hii imeelezea namna jamii nyingi za Waafrika walivyowakandamiza au kuwanyanyapaa watu waliozaliwa na ulemavu katika jamii.

Mwandishi ametumia ‘Zeruzeru’ Kama mfano tu wa wahanga wa mila na desturi zilizowataka wanajamii kuwafutilia mbali walemavu hao katika uso wa dunia hii.

Mwandishi amejaribu kuonesha baadhi ya mila zilizopo katika Jamii kuwa hazifai kuendelea kutumiwa kwani hazizingatii utu wa mtu. Tofauti za rangi au upungufu wa viungo vya mwili si kigezo cha kutotambua utu wa watu.

Katika riwaya hii, mwandishi anatuonesha maisha anayopitia Takadini kuwa yalijaa unyanyapaa, ubaguzi, uonevu na kudharauliwa n.k. Kuzaliwa kwa Takadini kulisababisha mgawanyiko mkubwa sana katika jamii kwani hakutakiwa na jamii nzima isipokuwa mama yake Sekai tu ambaye alilazimika kwenda uhamishoni ili kunusuru maisha ya mtoto wake. Takadini anatengwa na watoto wenzake, watu wazima na jamii nzima. Anakua katika maisha ya kutengwa sana.
Hata hivyo Sekai na baba Chivero ndio walibaki kuwa wazazi na marafiki wa kweli maishani mwake.

Je, Zeruzeru (sope) hakuwa na haki ya kuishi kama jamii yake ilivyoamini? Je, Zeruzeru hana nafasi katika ujenzi wa jamii mpya kama walivyo watu wengine?

Takadini katika maisha yake anatupatia majibu ya maswali yote haya. Takadini kama Zeruzeru (sope) aliweza kufanya shughuli mbalimbali kwa umaridadi kama watu wengine au hata kuwazidi watu wasiokuwa na ulemavu. Takadini alionyesha kuwa sope ni mtu kama walivyo watu wengine na kwamba wana hisia na haki ya kupenda na kupendwa. Takadini aliangukia katika penzi la dhati la Shingai.
Walifanikiwa kupata mtoto ambaye hakuwa Zeruzeru.
                              Kwa nini Zeruzeru wauliwe?

                              Kwa nini Zeruzeru watengwe?

                             Kwa nini Zeruzeru wadharauliwe?

                            Kwa nini Zeruzeru wavuliwe utu wao?

 Hakuna sababu ya msingi inayoweza kuhalalisha unyama wanaotendewa walemavu wote. Ni baadhi ya mila na desturi ndizo zimejaribu kuhalalisha hayo kwa muda mrefu. Jamii sasa inabadili mtazamo wake kuhusu zeruzeru na walemavu wote wanalindwa na kupewa fursa sawa na wengine ili utu na heshima zao ziweze kutambuliwa na kuzingatiwa na jamii nzima.


PITIO LA KITABU

  1. Familia ya mzee Makwati

edu.uptymez.com

Mzee Makwati alikuwa na wake wanne na wote aliwapenda sana. Mke wa kwanza alikuwa Sekai wa pili aliitwa Pindai, watatu Dadirai na wa mwisho ambaye alikuwa ni mdogo kuliko wote aliitwa Rumbiozai.

        Katika familia hii wake wa mzee Makwati wanaonekana wakibaguana wenyewe kwa wenyewe na pia wanakuwa hawaelewani huku wivu ukiwatawala.
Mfano, Mke wa kwanza alikuwa ni rafiki mkubwa wa mke wa pili na ndivyo hata mke wa tatu alikuwa rafiki wa mke wa nne ambaye ni wa mwisho. Sekai ni mke wa kwanza wa mzee Makwati na aliishi kwa miaka tisa pasipo ujauzito na hatimaye kupata ujauzito. Lakini ujauzito ule wa Sekai unaibua minong’ono ya chinichini kwa wake wenza na walimkejeli kwa kumwambia “ni ndama wangapi ambao ng’ombe wake mzee amepata kwa miaka minne iliyopita? Rumbiozai alihoji oh amezaa watatu kwa miaka minne. (Dadirai alijibu kwa sauti ya juu na Sekai akasikia).

       Kuwepo kwa imani za kishirikina hasa pale walipohisi ni kwa vipi Sekai anaweza kuishi muda mrefu pasipo kuwa na mtoto na mumewe. Pia tunaona kuwa chakula cha jioni kinaandaliwa na wake wote wanne wa mzee Mkwati lakini mzee Mkwati baada ya kuonja vyakula vyote ndipo anaishia kula chakula kilicholetwa na Sekai.

       Hatimaye Sekai anapata ujauzito na yeye analiona kitendo kile ni cha ajabu kwa kubeba mtoto mchanga katika mwili wake na anajiuliza je mtoto huyu atakuwa wa kike au wa wakiume na atakuwa na kasoro na mbaya zaidi kiumbe hicho kitakuwa binadamu au la maana ameshawahi kusikia kuhusu wanawake waliojifungua juu ya ujauzito ule wa mkewe. Sekai. Anatabiri juu ya ujauzito ule kuwa ni wa mtoto wa kike lakini mzee Makwati anakuja juu na kumwambia mkewe kuwa yeye haitaji tena mtoto wa kike bali anahitaji mtoto wa kiume. Hivyo Sekai anamhakikishia mumewe kuwa mtoto huyo atakuwa wa kiume na tena shupavu kama mzee Makwati mwenyewe.

       Pia tunaona juu ya msimamo alionao mzee Makwati allipokuwa akimwambia mkewe kwa kumuuliza, “Je, wewe siyo mke wa kwanza wa penzi la kweli? Vipi aibu yako isiwe yangu pia? Je, siyo Mimi niliyesimama imara kati ya wazazi wangu na wewe kwa miaka hii yote”? Na mkewe akajibu “Natambua hili sana maana umepigana nao kwa muda mrefu, nawe ulikataa kunirudisha kwetu maan hapo sina dada wa kuchangia naye mkeka, nashukuru sana mume wangu kwa kunifichia aibu yangu.

  1. Furaha kubwa kwa Sekai

edu.uptymez.com

Muda wa mwisho wa ujauzito wa Sekai ulikaribia na ndipo rafiki yake, mke mwenza Pindai anamsaidia kazi za nyumbani. Amai Pedzisai ni mzee aliyekuwa kipenzi cha Sekai na aliweza kuwa karibu sana na Sekai mpaka alipokaribia kujifungua. Sekai alipata maumivu makubwa ya uchungu kuliko maumivu yote aliyowahi kuyapata, mbali na maumivu hayo lakini alitarajia kuwa na furaha kubwa siku chache zijazo.

     Hatimaye Sekai alijifungua mtoto wa kiume. Taarifa hii ilipelekea furaha kubwa kwa mume Makwati. Lakini mtoto huyu aliyezaliwa aligundulika kuwa ni Sope(zeruzeru) na hata Sekai aligundua hilo na ndipo Sekai anaonyesha kuwa na woga juu ya mtoto yule lakini kwa upande mwingine anaonyosha ujasiri wake kwa kusema, “Lazima mtoto aishi maana nimesubiri kwa muda mrefu na nimeshateseka sana juu yake, hivyo mtoto huyu ni wangu na wala sitamuachia mtu”. Ambuya alimwambia, “hujui ulisemalo hivyo usihofu maana uzazi umeshafunguka na watafuata watoto wengine”.

     Mzee Makwati anapata taarifa juu ya mtoto aliyezaliwa kuwa ni sope(zeruzeru) naye anaonyesha kuchukizwa na kiumbe hicho na alihoji kwa mkewe katika hali ya maswali ya mfululizo mfano, “Huo ni uchawi au ni laana ya mizimu? Na kwa nini huyo Sope yungali nasi”?, maswali haya yalimtatiza Sekai katika kuyajibu, na ndipo mzee Makwati alitoa suluhisho kwa kusema wazee ndio watatoa suluhisho la kuwepo au kutokuwepo kwa mtoto yule.
Mganga mashuhuri aitwaye Zviyedzo anashirikishwa katika kutatua tatizo lile la mtoto ambaye ni Sope.

  1. Gumzo dhidi ya mtoto Zeruzeru

edu.uptymez.com

Kuzaliwa kwa mtoto wa ajabu pale kijijini kulizua gumzo kubwa na habari kuhusu mtoto huyo zilienea kwa haraka kijijini hapo hivyo kila mtu alishikwa na butwaa.

Wake wenza na Sekai walimkejeli kwa maneno mabaya na wengine walionyesha chuki zao lakini ilikuwa tofauti kwa Pindai ambaye alionyesha upendo kwa mke mwenza huyo.

     Pindai na Pedzisai walimtembelea Sekai na waliweza kujadili mambo mbalimbali zikiwemo mila na desturi za hapo kijijini . Pia waliweza kumuuliza Sekai ni kwanini aliendelea kuwa na mtoto yule na hivyo walimueleza kuwa alikuwa akipinga mila na desturi zao hapo kijijini na kutojulikana kwa ufumbuzi wa mtoto yule kulimpelekea Sekai kuwa na mawazo mengi yasiyo na kikomo, hata mzee Makwati pia naye alikuwa na mawazo mengi juu ya mtoto yule aliyezaliwa akiwa Sope.

     Mzee Makwati anakasirika kwa kuona mtoto yule aliye Sope na anamshutumu mkewe labda ametembea na mwanaume mwingine hivyo amevunja mila ma desturi zao. Sekai aliumizwa sana na tuhuma hizo maana alijiona hana maana tena mbele ya mumewe na anajihisi aliyetelekezwa zaidi wakati huo. Mtihani mkubwa ulikuwa kwa Sekai na alichokuwa akisubiri ni hukumu kutoka kwa wazee juu ya yeye na mwanae kuendelea kuishi au kutoendelea kuishi.

    Mikakati mikubwa ilipangwa na Sekai ili kunusuru kifo chake pamoja na mwanaye hivyo alipanga kutoweka upesi katika kijiji kile, lakini uamuzi wake ulihitaji ujasiri mkubwa na ungeweza kuleta matumaini ya kuishi maisha mapya kwa Sekai na mtoto wake.

     Alfajiri ilipofika, Sekai alijiandaa kwa safari, alifungasha vitu vyote ambavyo vilikuwa muhimu katika safari yake na bila kusahau zana za kujilinda dhidi ya wanyama wakali ambazo ni ngao na mkuki. Kabla ya kuanza safari, Sekai aliketi na kuiambia mizimu matatizo yake na akaomba akingwe na mambo yote ya hatari mbele ya safari yake.

     Wakati alipo wasiliana na mizimu, punde jina likamjia moyoni aliweza kumpa jina hilo mtoto wake ambalo ni TAKADINI, ni jina ambalo hakuwahi kulisikia mahali popote pale. TAKADINI maana yake ni “Sisi tumefanya nini?” Jina hili lilisawiri vyema mambo yote yaliyomtokea Sekai wakati wa uzazi wa mwanae na huu wa sasa wenye hatari zaidi kwake.

  1. Safari ya Sekai

edu.uptymez.com

Alfajiri na mapema Sekai alianza safari yake kimyakimya toka kibandani mwake.

Alimchukua mwanae Takadini na vifurushi alivyoviandaa kwa ajili ya safari bila kusahau mkuki na ngao.

     Sekai alivuka milima, mabonde na tambarare akielekea asikokujua. Kijiji alichotoka Sekai aliacha gumzo kubwa juu yake ambapo wengine walisema, “Labda alikwenda kujinyonga au amekwenda kujitosa majini.

     Habari za kutoweka kwa Sekai zilienea kijiji kizima na ndipo Mtemi Zvedi aliitisha mkutano ili kujadili ni wapi aloko kwenda Sekai na ndipo Mtemi alitoa agizo la kumtafuta Sekai popote pale kuzunguuka kijiji chote.

     Katika safari yake Sekai anakutana na mzee Chivero na anamueleza mkasa wote uliompata na lengo la yeye kutoroka. Mzee Chivero anamkaribisha Sekai katika kijiji chake na anamtambulisha kwa mtemi wa kijiji aitwaye Masasa. Katika kijiji waliweza kumjadili Sekai na mtoto wake ingawa ilikuwa vigumu kumkaribisha Sekai katika kijiji chao lakini hatimaye walimruhusu. Mzee Chivero ndiye aliyekuwa mlezi mkuu wa Sekai na mtoto wake.

  1. Maisha mapya ya Sekai

edu.uptymez.com

Ujio wa Sekai katika kijiji kile kipya ulikuwa gumzo kijiji chote. Wazee wa kijiji walikutana na kuweza kumjadili mgeni huyo aliyeingai katika kijiji chao. Wazee hao waliongozwa na mtemi Masasa.

     Kulikuwa na imani zilizofuatiana juu ya ujio wa Sekai na mtoto wake maana walijiuliza maswali mengi pasipo kupata majibu sahihi. Na hatimaye walifikia tamati na wote walikubaliana kutomfukuza mgeni huyo maana mizimu ya kijijini hapo ilipinga kumfukuza mgeni yeyote atakayeingia kijijini hapo kinyume na hivyo kungepelekea laana kubwa toka kwa mizimu ya hapo kijijini.

     Matumaini ya kuishi kwa Sekai na mtoto wake aliyekuwa Zeruzeru yalirejea upya baada ya kukubaliwa na wazee wa kijiji kuishi katika kijiji kile alichofikia.

     Sekai aliweza kujengewa makazi yake pamoja na mwanae na kujishughulisha na shughuli zote za uzalishaji kama wanakijiji wengine.

Baadhi ya wanakijiji walimtenga Sekai na mtoto wake hasa upande wa wanawake wenzake. Lakini hili halikuwa tatizo kwake bali yeye alifurahia maisha mapya na yenye matumaini na aliweza kumshukuru sana mzee Chivero kwa usamalia wake wa kumsaidia yeye na mtoto wake ambaye ni Zeruzeru.

  1. Sekai apata rafiki

edu.uptymez.com

Sekai alikuwa mwanamke mchapakazi na hodari kama wanawake wengine hapo kijijini. Mzee Chivero alipata msaada mkubwa kutoka kwa Sekai kwa kufanya shughuli za nyumbani kwa mfano, kuandaliwa chakula.

     Sekai alikuwa mpweke na mwenye huzuni maana wanawake wenzake walimtenga na mbaya zaidi alipokuwa akitoka shamabani njiani alikuwa akikutana na wanawake wenzake. Wanawake wajawazito hawakupenda kupishana naye na punde walipomuona walijifunika mikono yao usoni au walirudi nyuma ilimradi tu wasikutane uso kwa uso na Sekai. Mzee Chivero alitambua hilo na hivyo alikwenda kuomba msaada wa ufumbuzi wa tatizo hilo kwa mtemi Masasa na ndipo mtemi alimruhusu mzee Chivero amchukue Tendai ili amtambulishe kwa Sekai ili awe rafiki yake.

     Tendai alikuwa mke wa mwisho na mdogo wa mtemi Masasa. Mzee Chivero alimtambulisha Tendai kwa Sekai. Hatimaye, Tendai ndiye aliyekuwa rafiki mkubwa wa Sekai na waliweza kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii.

     Takadini sasa alifikia umri wa kuweza kukaa na hata kumtambua ipasavyo mama yake. Tendo hili lilimuongezea furaha na matumaini makubwa Sekai.

  1. Tukio la ajabu lamtokea Sekai

edu.uptymez.com

Siku moja alikuwa akirejea nyumbani toka shambani njiani aliona vijana ambao walikuwa wakirina asali.

     Ghafla kundi la nyuki lilimvamia na ndipo Sekai alimtupa mtoto kichakani na yeye alijitosa majini ili kunusuru maisha yake pamoja na mwanae. Sekai alifanikiwa kuokoa maisha yake na ya mtoto pia ingawa walipata maumivu makubwa ya kuumwa na baadhi ya nyuki.

     Mzee Chivero alipata taarifa hizo na aliweza kutoa msaada wake kwa kuwatibu na alitumia dawa za mitishamba na hatimaye Sekai na mwanae walirejea katika afya yao ya kawaida kama ilivyokuwa awali.

     Lakini kwa Takadini haikuwa hivyo kwani alidhurika sana na aliweza kupata kilema cha maisha katika mguu wake ambacho kilitokana na kutupwa kichakani na mama yake katika harakati za kunusuru maisha yake. Huzuni kubwa ilimjia tena Sekai na aliwaza mengi juu ya mtoto wake. Pia alipatwa na uchungu na alijiuliza maswali mengi kwa kuhisi ameikosea mizimu yao kwa yeye kutoroka kijijini kwake.

     Lakini Sekai alijikaza na aliamini kuwa yeye ni shupavu na yote hayo aliwaachia mizimu, hivyo muda mfupi alirejea katika hali yake ya kawaida kama alivyokuwa awali.

  1. Maisha ya Takadini

edu.uptymez.com

Takadini alikuwa na furaha kubwa bila kujali hali yake na wakati huo alianza kutambaa kwa kuvuta mguu mbovu wa kushoto. Pia. Takadini alitaabika sana wakati wa mwanga mkali na joto la jua lilimuumiza kiasi ambacho shingo yake ilienea michubuko. Kwa mapenzi ya mzee Chivero, Tendai na mama yake, Takadini alijiona ametimia kwani waliongea naye, wakacheza naye na wakamfanya ajisikie anapendwa na mwenye furaha.

     Takadini alitengwa na watoto wenzake na pia walimdharau kwa kumwambia yeye alikuwa ni Sope na tena amelaaniwa.

     Mzee Chivero alipokuwa akielekea msituni aliongozana na Takadini huko msituni alimfundisha jinsi ya kufahamu dawa za mitishamba na matumizi yake mbalimbali.

     Takadini alionekana kuwa ni mtoto mwelevu mwenye kupenda kufahamu mambo mbalimbali. Siku moja Takadini alihuzunika sana pale alipoambiwa na watoto wenzake kuwa yeye ni Sope na tena amelaaniwa, ndipo kitendo kile kilimfanya Takadini akose raha kabisa. Mzee Chivero na mama yake walimfariji Takadini na ndipo mzee Chivero alimfariji kwa kumwambia, “Mbuyu sio mwembamba na mzuri kama miti mingine, lakini ni imara na unaishi maisha marefu kuliko miti yote msituni na ni mti wenye matumizi makubwa”. Hivyo Takadini alipofikiri akajilinganisha na mti ule kama ulivyotofautiana na miti mengine ndivyo yeye alivyotofautiana na wengine.

     Akaongeza kwa kumwambia tena “Hakika wewe ni wa kipekee, na ndiyo maana upo tofauti nao, lakini bado hawajui kuwa wewe ni pekee kiasi gani.

  1. Maisha ya Takadini

edu.uptymez.com

Siku moja mzee Chivero anamletea Takadini mbwa ambaye alikuwa ni rafiki sana na Takadini hasa alipokuwa akienda msituni peke yake. Mzee Chivero alitambua hatokuwa na Takadini siku zote maishani hivyo mbwa yule angekuwa mlinzi mkubwa wa Takadini, mbwa huyo aliitwa Shumba.

     Takadini alipenda sana kusikiliza hadithi mbalimbali zilizokuwa zikisimuliwa na wazee katika dare kama vile Tsuro mwenye busara. Takadini alipofikisha miaka kumi na tatu hali ya afya ya mzee Chivero ilidhohofu na alianza kukohoa muda wote, ndipo alianza kumuagiza Takadini dawa za kumletea toka msituni na Sekai aliendelea kumtunza vyema.

     Takadini alijifunza kutabiri kwa kutumia mifupa na kujua sifa mbalimbali za miti shamba ambayo mzee Chivero alikusanya maishani katika kutibu maradhi mabalimbali.

     Katika kijiji hicho kulitokea matukio makubwa mawili, kwanza ni sherehe ya mavuno ambayo iliambatana upigaji wa mbira na pia watu hucheza wakubwa kwa watoto, wanaume kwa wanawake.

     Takadini alivutiwa sana na upigaji mbira lakini aliwaza ni nani atakayemfundisha maana alikuwa hana rafiki. Lakini hakukata tamaa ndipo akamueleza mzee Chivero. Mzee Chivero alimahidi kumtafutia mtu atakayemfundisha.

     Tukio la pili katika kijiji hicho ni kutokea kwa mvua kubwa na kufariki kwa wazee maarufu kijijini hapo. Alianza kufariki mtemi Masasa ambaye alikuwa kiongozi wa kijiji kile na ndipo akafuata mzee Chivero ambaye alkuwa mganga mashuhuri kijijini hapo.

     Wanakijiji wotw walihuzunika sana Sekai na Takadini walihuzunika sana baada ya kuondokewa na mzee Chivero ambaye alikuwa ndio mlezi wao na mwenyeji wao mkuu. Baada ya miezi kadhaa Sekai na mwane Takadini walirejea katika hali ya kawida na kuendelea na shughuli za kila siku.

  1. Maisha ya Takadini baada ya kifo cha mzee Chivero

edu.uptymez.com

Ulipita mwezi baada ya kifo cha mzee Chivero, ndipo siku moja mcheza mbira maarufu alipomtembelea Sekai na kumfahamisha juu ya ujio wake pale nyumbani kumfundisha Takadini kupiga mbira. Kwani aliagizwa na mzee Chivero kabla hajafariki. Takadini aliitwa na akaelezwa na baba Kutukwa kuhusu kumfundisha jinsi ya kupiga mbira. Takadini allifurahi sana na muda mfupi alianza mazoezi hatimaye alikuja kuwa hodari wa kupiga mbira.

Mzee Kutukwa alikuwa ni mzee mwenye busara kwani alimpenda sana mtoto yule aliye mpweke na alimsaidia sana kwani siku moja aliwaza kumsaidia Takadini ndipo alimtengenezea mti mzuri ambao ungemsaidia Takadini wakati wa kutembea kwani hapo mwanzo alipata shida sana kwa kutembea kwa kurukaruka.

     Takadini alijawa na furaha baada ya kukabidhiwa mti ule na alianza kutembea kwa haraka sana, na huku akiwasalimu rafiki zake njiani, na wao walimshangaa sana.

     Furaha na shukrani vilimjia Takadini katika nafsi yake na ndipo alichukua mbira akaanza kupiga huku akiimba wimbo mpya ambao ulimjia kama taswira akilini mwake:

“Nawashukuruni baba zangu, Chivero kwa kunikamilisha, kwa kunipa fruraha kwa kunijaza moyo wangu kwa muziki na amani”.

Sekai alivutiwa sana na wimbo huo uliokuwa mpya masikioni pake hivyo naye aliishukuru mizimu kwa furaha aliyonayo.

  1. Tukio la kusikitisha latokea kijijini

edu.uptymez.com

Miezi sita ilipita baada ya Takadini kuanza kupiga mbira. Vijana wote wa kijijini hujishugulisha na uchungaji wa mifugo yao na pindi wawapo machungani huonyeshana ubabe wa kupigana ili kujua nani zaidi.

     Ilikuwa ni tofauti na siku zote siku hiyo waliendekeza mchezo wao kama kawaida yao kumbe siku hiyo alitokea simba mkubwa na akamla ng’ombe mmoja ambaye ni maksai. Kitendo hicho kiliwasikitisha sana wanakijiji hivyo walijawa na woga dhidi ya simba huyo.

     Wanakijiji wanapanga kuingia msituni ili kumsaka simba huyo na hatimaye wanafanikiwa kumuua simba huyo. Baada ya ushindi huo, wanakijiji wanafanya sherehe kubwa ili kujipongeza kwa ushindi huo.

     Takadini alikuwa mmoja kati ya wapigaji mbira katika sherehe hiyo. Lakini baadhi ya watu walikasirishwa na tendo la kumhusisha Takadini ambaye alikuwa ni Sope (zeruzeru) watazamaji na wachezaji siku hiyo walifurahishwa sana na upigaji mbira wa Takadini na wimbo wake ambao watu wote waliupenda.

      Baadhi ya wasichana walivutiwa sana na uhodari wa Takadini akiwepo msichana mmoja aitwaye Shingai.

     Shangai alitoke kuvutiwa sana na Takadini hivyo alitumia kila mbinu ilimradi awe karibu na Takadini.

Siku moja Shingai aliteka maji mtoni na kumpelekea Sekai nyumbani kwake na ndipo Sekai anastaajabu kwa tendo lile lakini Shingai anathibitisha kwa kumwambia amejitolea tu kwani kwake anaona si vibaya kumsaidia mtu mkubwa.

     Hatimye habari zilienea kijiji kizima kuhusu kitendo cha Shingai alichofanya.

Wazazi wa Shingai walichukizwa sana. Wazee wa kijiji nao waliweza kujadili hili na ingawa hawakufikia muafaka wa tukio hilo.

  1. Gumzo kijijini dhidi ya Takadini

edu.uptymez.com

Tendai anamtembelea Sekai nyumbani kwake na wanajadili juu ya Takadini na Shingai. Baada ya Shingai kuzuiliwa kutokewenda tena nyumbani kwa Sekai, hivyo Shingai alikuwa mpweke sana na mwenye mawazo juu ya Takadini. Hivyo ndivyo ilivyokuwa hata kwa Takadini kwani alijihisi kukosa amani.

     Shingai alipendwa sana na kijana aitwaye Nhamo, lakini Takadin na Nhamo walikuwa maadui toka utotoni.

     Ilifanyika tena sherehe nyingine kubwa hapo kijijini maalumu kwa kumkumbuka marehemu mzee Chivero na Takadini alichaguliwa katika kupiga mbira. Takadini alionyesha umakini wake hasa pale alipoimba wimbo wake mwenyewe wa kumtunza mzee Chivero. Sauti yake ilikuwa nzuri na kila mtu alivutiwa naye na kusahau kama aliyecheza na kuimba ni Sope(zeruzeru). Shingai naye hakuwa mbali, bali naye alikuwepo katika sherehe hiyo pia hata Nhamo alikuwepo akifuatilia nyendo za Shingai na Takadini.

     Hatimaye Nhamo aliweka mambo wazi juu ya azma yake ya kumuoa Shingai na alimtuma munyai (mshenga) akatoe taarifa nyumbani kwa akina Shingai lakini Shingai hakuvutiwa na Nhamo bali alivutiwa na Takadini.

     Siku moja Nhamo alikwenda nyumbani kwa akina Takadini na akamtahadhalisha aachane na Shingai vinginevyo atampiga. Kitendo hiki cha kitisho kilimnyima raha Takadini lakini alipiga moyo konde.

     Chido naye alikuwa msichana ambaye naye alivutiwa Sana na Nhamo hivyo Chido na Shingai alikuwa hawapatani. Swala hili lilimjengea sana hofu Shingai kwani hakupenda kuchangia mume mmoja na Chido. Shingai alitamani awe na ujasiri kama wa Sekai ambapo alipingana na wazee wa kijiji na hata Takadini akakua baada ya kuuawa.

     Wakiumizwa na haja ya kuficha hisia zao za kweli, Shingai na Takadini walitafuta mbinu za kuweza kuonana. Tambudzai alikuwa ni rafiki wa Shingai na alikuwa akimsaidia sana Shingai pindi wasichana wenzake walipomsema baada ya yeye kuhisiwa kuwa ana mahusianao na Takadini.

  1. Furaha ya Takadini.

edu.uptymez.com

Ulibaki mwezi mmoja kabla ya ndoa kati ya Nhamo na Shingai. Takadini alitumia muda mwingi kujifariji na mbira yake kwa kumkomoa mpenzie. Kabla ya ndoa, mzee maarufu aitwaye Makaure alifariki dunia hivyo wanakijiji walihuzunika sana.

     Siku moja katika kibanda chake Takadini alisikia mtu akifungua mlango na alipotahamaki alimuona Shingai akiingia ndani mle katika usiku wa kiza. Shingai alimkaribia Takadini na akavuta gudza na wakajikuta wanafanya tendo la ndoa. Jua lilipochomoza Shingai hakuonekana kwao na walipomtafuta walimkuta kwa akina Takadini.

    Familia ya akina Shingai ilimtenga kuanzia siku ile lakini Sekai hakumfukuza Shingai nyumbani kwake. Wazee wa kijiji waliwajadili sana Shingai na Takadini lakini walifikia tamati kwa kusubiri kitakchoendelea.

Nhamo aliamua kumua Chido badala ya Shingai. Chido na Nhamo wakaungana kumchukia Takadini. Chido alimchukia sana Shingai baada ya kujulikana ana mahusiano na Takadini.

     Baada ya siku chahe Shingai aligundulika kuwa ni mjamzito. Muda mfupi alijifungua mtoto wa kiume ambaye si Sope(Zeruzeru) tena, bali alikuwa kama watoto wengine. Sekai alijawa na furaha na kujisemea moyoni, “kumbe Takadini ni rijali”.

    Tendai alimshukuru sana Sekai na alimwambia kuwa yeye na Takadini wameleta mabadiliko kijijini hapo hasa katika kumdharau mtu aliye na ulemavu kama Takadini. Sekai alimshukuru rafiki yake na alipanga kurejea na familia yake katika kijiji chake cha nyumbani.

     Je, taswira hiyo ya mila dhidi ya Masope(mazeruzeru) ingepokelewaje na jamii ya mama yake Takadini pindi watakaporejea?


C. MAUDHUI

DHAMIRA KUU:

Ukombozi wa kiutamaduni

Dhamira kuu katika riwaya hii ni ukombozi wa kiutamaduni.

Mwandishi anaonekana kusukumwa na tatizo la jamii kukumbatia mila na desturi zilizopitwa na wakati.

       Katika jamii kuna mila na desturi zimetumika kama chombo cha ukandamizaji. Mila na desuri zimeelezwa kutumika kukandamiza wanawake na watooto katika vipengele vifuatavyo:

  1. Ndoa
  2. Mirathi
  3. Uhai
  4. Maamuzi
  5. Mgawanyo wa kazi
  6. Mgawanyo wa mapato na umilikaji wa mali
  7. Elimu
  8. Utu

edu.uptymez.com

Waandishi wengi kama vile Ebrahimu Hussein katika tamthiliya yake ya Kwenye Ukingo wa Thim, Penina Mhando katika pambo, N.k. wamejadili namna baadhi ya mila na desturi zinavyotumika katika ukandamizaji wa wanawake, watoto na walemavu.

     Mwandishi wa riwaya hii, anaonesha namna mila na desturi mbaya zinavyotumika kuwakandamiza wanawake na makundi mengine ya wasiojiweza. Mfano wa mila na desturi zinazotishia uhai, haki na maisha ya watoto walemavu kama Takadini, kijana aliyejaliwa akiwa zeruzeru ambaye jamii yake iliazimia kumuua siku ya pili baada ya kuzaliwa kwake. Katika ukuraasa wa 19 mwandishi anasema.

Sekai alimpenda Makwati – siku zote alimpenda . Na sasa anamuacha aamuliwe na wazee kwa sababu ameshindwa kumpatia aina ya mtoto aliyetaka… mtoto huyu asiye na msaada alimtegemea yeye kama tu alitaka aishi. Katika kijiji hiki, kati ya watu wa Makwati, Zeruzeru hakuwa na nafasi”.

Kauli hii inathibitisha kuwa jamii haikuthamini mtu ambaye alikuwa ni mlemavu. Wazee wa kijiji ndiyo walikuwa wasimamizi wa mila na desturi hizi za kikatili. Takadini kama mlemavu maisha yake yaliokolewa na mama yake ambaye aliamua kuvunja shina na miiko iliyowekwa ili kuangamiza Zeruzeru.

     Uonevu wa mila na desturi huakuwalenga watoto tu, bali ukandamizaji uliwagusa pia wanawake katika jamii. Mwandishi anamuonesha Sekai kama mhanga wa mila na desturi zinazokandamiza wanawake. Baada ya kuzaa mtoto aliyekuwa na ulemavu (zeruzeru) na kukataa mwane asiuawe, Sekai naye kifo kilimkabili kwa mujibu wa mila na desturi za kabila lao. Haya yanaweza kuthibitishwa na maelezo ya Makwati akimtahadharisha Sekai, alisema,

         “Lakini Sekai kama wataamua mtoto auawe, hata nawe utauawa kwa sababu ya kupinga sheria za kale”.

Kauli hii inaonyesha namna wazee walivyotumia mila na desturi ‘katili’ kutoa hukumu kubwa ambayo Mungu pekee angestahili kuitoa na si mwanadamu yeyote. Hukumu ya kukatisha maisha ya binadamu ni ya ukatili. Wazee waliazimia kutekeleza sheria, mila na desturi za kabila lao bila kujali madhara yake.

Je, haitupasi sasa kuleta ukombozi wa kiutamaduni kwa kurekebisha baadhi ya mila na desturi zilizopitwa na wakati? Wakati umefika sasa kwa jamii kuliona hilo. Kuwa tayari kuzifanyia marekebisho baadhi ya mila ambazo zinatuumiza wenyewe. Kwa gharama yoyote ile tunapaswa kutetea haki, uhuru na utu wa watu wote dhidi ya mila na desturi zinazokiuka haki, uhuru na utu wa mtu.

Mwandishi anasema,

      Sekai alikwishaamua: lazima aondoke asubuhi itakayofuata.Sekai hakuwahi kutenda jambo kinyume na Makwati wala mila zao, isipokuwa kwa hili,         kulilia uhai wa mtoto wake. Uamuzi wake ulikamilika kwa usahihi na ushwari, sifa ambazo hakujua kuwa alikuwa nazo.”

Jamii inapaswa kuwa jasiri kama Sekai aliyeamua kuvunja, sheria zilizokuwa zimepitwa na wakati.

        Mwandishi anaonesha pia namna mila na desturi zinavyoingilia hata masuala ya ndoa. Mwanamke alinyimwa haki ya kuchagua mtu anayempenda kuwa mume wake, kama inavyoonekana kwa Shingai. Hata kivyo Binti huyu pia alipigania haki na uhuru wake kwa kumkataa mchumba aliyechaguliwa na wazazi wake. Katika kutetea uhuru na haki yake, Shingai anasema,

      “Huyu ndiye mtu ninayetaka aniowe. Hakuna aliyeniuliza kama nampenda Nhamo. Wewe na baba mlikuwa na hamu ya kuniozesha katika familia ya   Manyamombe hata matakwa yangu hayakusikilizwa. Sasa nimechagua . Nakuomba msamaha wako mama, unaweza ukaniua kama ukitaka, lakini katu kwa Nhamo siendi hata kama angekuwa nami sasa”.(uk118).

Je, ni nani ataleta mabadiliko kama siyo sisi wenyewe tunaoathirika na milahizi mbaya? Shingai anatuonesha njia kuwa ukombozi wowote ule ni lazima tuwe tayari kujitoa mhanga kama alivyofanya Sekai na Shingai ambao walileta mabadiliko katika jamii zao. Tendai anashuhudia hilo kwa kusema.

     “….Sekai. Wewe na Takadini mmebadilisha mambo mengi kijijini hapa. Kwa sasa, sifikirii kwamba kuna mtu yeyote atakayekuwa na moyo wa kuharibu watoto wachanga Masope au wenye ulemavu. Ahsante nyingi kwako na Takadini na kwa baba Chivero. Ndiyo hurejea huko baada ya muda mrefu hivi huenda kukawapa funzo kama hili pia…..”(uk.126).

Kwa ujumla mwandishi amejaribu kuonesha baadhi ya mila na desturi zenye walakini katika jamii nyingi za kiafrika na ameonesha njia  za kuondoka nazo ili kuleta ukombozi.

Dhamira Ndogondogo

Katika riwaya hii, kuna dhamira mbalimbali ambazo zimeijenga dhamira kuu. Dhamira hizo ni pamoja na hizi:

  1. Mapenzi
  2. Ndoa
  3. Imani potofu
  4. Upendo
  5. Ujasiri
  6. Umoja na mshikamano
  7. Elimu
  8. Nafasi ya mwanake

edu.uptymez.com

Dhamira hizi zote zinajenga dhamira kuu ya ukombozi wa kiutamaduni kwa kuonesha sheria, mila, na deturi zinavyogusa dhamira zote hizo.

  1. Mapenzi

edu.uptymez.com

Mapenzi ni dhamira ambayo imejadiliwa katika riwaya hii ya Takadini. Mwandishi amejaribu kuonesha kuwa katika jamii kuna aina mbili ya mapenzi. Mapenzi ya dhati na mapenzi yasiyo ya dhati. Mwandishi anaona kuwa mapenzi ya dhati ndiyo humfanya mtu aheshimu wengine, ajali haki na utu wa mtu, ajisikia uhuru na kukwepa kupandikiza chuki na badala yake humfanya ahimize ushirikiano, umoja na upendo.

     Katika riwaya hii ya Takadini tunaona mapenzi ya dhati kati ya Takadini na mama yake. Takadini na mzee Chivero, Takadini na Shingai, Sekai na Pindai, na Sekai na mzee Chiro.

       Mapenzi ya Sekai kwa Takadini (mwanae) yalikuwa ya dhati kwa sababu Sekai alikuwa radhi kufa ilimradi mwanae Takadini asipate madhara. Sekai alimlinda mwanae wakati wote, Sekai alikabiliana na mumewe katika hali ya kumlinda Sekai anasema,

           “Ni mtoto wangu wa kwanza niliyemsubiri kwa miaka mingi. Siwezi kukubali kumpoteza. La humataki, nirejeshe kwetu au hata msituni, lakini usije kunilazimisha nitengane naye. Nitajitoa mhanga kwa ajili yake”.

Haya ni mapenzi ya dhati ya mama na mtoto wake. Mama alijitoa mhanga kumlinda mwanae katika hali ya hatari. Alijua fika nini kitamkabili mbeleni kwa kufanya mambo kinyume na taratibu za kabila lake.

         Mapenzi ya dhati yanajitokeza kati ya Takadini na Shingai. Takadini ni kijana mwenye ulemavu wa aina mbili (mguu na ni zeruzeru) hivyo alitengwa na jamii.

Katikati ya upweke wake ambao umetokana na ulemavu anapumzishwa machungu hayo na binti aitwae Shingai . Shingai alikuwa na mapenzi ya dhati kwa Takadini. Ingawa wazazi wake walimkataza na kumchagulia mchumba, Shingai alikuwa na msimamo na kuelezea wazi hisia zake kwa wazazi wake. Katika hali ya kutetea penzi lake la dhati Shingai anasema,

        “Huyu ndiye mtu ninayemtaka anioe. Hakuna aliyeniuliza kama nampenda Nhamo. Wewe na baba mlikuwa na hamu ya kuniozesha katika familia ya Mnyamombe hata matakwa yangu hayakusikilizwa. Sasa nimechagua. Nakuomba msamaha wako mama, unaweza ukaniua kama ukitaka, lakini katu kwa Nhamo siendi hata kama angekuwa namI sasa.”(uk118).

Uamuzi huu unadharirisha kuwa mapenzi ya dhati hayachagui rangi, kabila, mali au vitu vingine. Mbali ya kukanwa na wazazi wake Shingai hakubadili msimamo wake. Alitunga mimba na kuzaa mtoto. Shingai anadhihirisha penzi la dhati kwa Takadini.

          Mapenzi mengine ya dhati ni kati ya mzee Chivero na Sekai. Wakati wa kutoroka, Sekai anakutana na mzee Chivero na anamweleza mkasa wote uliompata na lengo lake yeye kutoroka. Mzee Chivero anamkaribisha Sekai katika kijiji chake na anamtambulisha kwa Mtemi wao. Mzee Chivero ndiye aliyekuwa, mlezi mkuu wa Sekai na mtoto wake hadi kifo kilipomchukua. Hivyo inaonesha wazi  kuwa mzee Chivero alikuwa mkarimu na mpole kwa wageni na hivyo alikuwa na mapenzi ya dhati.

          Mapenzi kati ya mzee Chivero na Takadini vilevile yalikuwa ya dhati. Mzee Chivero alimpenda sanaTakaini kwani alimfundisha mambo mbalimbali kama vile uwindaji, alimfundisha jinsi ya kufahamu dawa za mitishamba na matumizi yake mbalimbali. Kila wakati Takadini alipokuwa na huzuni alifarijiwa na mzee Chivero.

           Vilevile mapenzi kati ya Sekai na Pindai yalikuwa ni ya kweli. Pindai alikuwa mke mwenza wa Sekai na alimpenda sana kuliko wake wenzake ambao kila wakati wakilimsengenya Sekai kwa sababu ya kutopata mtoto. Lakini wakati wote Pindai alifariji Sekai kutokana na kusengenywa na wake wenza.

         Mapenzi mengine ya kweli ya dhati ni kati  ya Sekai na Tendai. alikuwa mke wa mwisho na mdogo wa Mtemi Masasa. Tendai ndiye alikuwa rafiki mkubwa wa Sekai na aliweza kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii.

          Kwa upande wa mapenzi ya oungo yasiyo ya dhati nayo yamejadiliwa katika riwaya hii, kwanza mapenzi ya uongo ni kati yam zee Makwati kwa mtoto wake Takadini. Mzee Makwati alikasirishwa na kitendo cha kuzaliwa takadini akiwa Zeruzeru, kutokana na kitendo hicho mzee Makwati alifuata mila na alitaka Takadini auawe kwani aliona kuzaliwa kwake ni kama kuleta balaa katika familia yake, lakini mama yake Sekai alitoroka na mtoto ili asiuawe.

         Mapenzi ya uongo ni kati ya mzee Makwati na Sekai baada ya kujifungua mtoto Zeruzeru. Mzee Makwati alikasirishwa kwa kuona mtoto yule na alimshutumu mkewe kuwa alitembea na wanaume wengine hivyo alivunja mila na desturi zao. Sekai aliumizwa sana na tuhuma hizo maana alijiona hana maana tena mbele ya mumewe na alijihisi ametelekezwa zaidi  wakati huo.Kutokana na kitendo hicho cha kutelekezwa na mume wake sekai aliamua kutoroka.

         Mapenzi mengine ya uongo ni kati ya Dadirai na Rumbiozai kwa Sekai, hawa walikuwa ni wake wenza wa Sekai na waliishi maisha ya kumsengenya Sekai kila wakati. Hawa hawa kuwa na mapenzi ya kweli kwa Sekai, kwani waliishi kwa kumbaguana Sekai walikuwa na wivu naye na matokeo yake kukawa na mvurugano wa kifamilia.

  1. Ndoa

edu.uptymez.com

Ndoa ni makubaliano kati ya watu wawili wapendanao ambao wameamua kuishi kama mume na mke. Maamuzi ya juu ya nani awe mume au mke ni juu ya wale wapendanao. Mila na desturi zimeingilia ndoa za watu katika jamii madhara yake yamekuwa makubwa: Ndoa zimevunjika na hata kukosekana kwa amani.

Katika riwaya hii , Shingai alilazimishwa kuolewa na Nhamo. Kitendo hiki hakikumfurahisha Shingai. Alisema

          “Ama! siyo kama ninamchukia Nhamo, la hasha. Isipokuwa sidhani kama nitakuwa na furaha kuishi naye.” (uk.110).

Ingawa mila na desturi ziliwabana watoto wa kike kuwa na uhuru lakini ukweli ni kwamba mila hizo zilisababisha ndoa nyingi kutokuwa na furaha. Shingai anasisitiza.

            “Sikumwambai kufanya hivyo na simtaki. Nataka waniache peke yangu ili naimue mwenyewe…..” (uk115)

Pia mwandishi wa riwaya hii amegusa suala la ndoa za mitala. Mwandishi ameonesha kuwa ndoa za mitala ni desturi ambayo jamii inapaswa kuachana nayo. Mwandishi ameonesha namana ndoa za mitala zinavyochangia kuleta mifarakano katika familia. Mfano mzuri ni namna wake zake Makwati walivyokuwa wakiishi kwa kusengenyana na uadui mkubwa ulizuka miongoni mwao. Haya yanajitokeza (uk 1- 20). Katika (uk.3) Pindai anasema,

           “Si ajabu wale wawili wanahofu utapata mtoto wa kiume…. Wanaamini kuwa Makwati atahamishia mapenzi na uangalizi kwa mtoto huyo. Pia, mume wetu atazidisha mapenzi kwako. Aidha wana imani kwamba umepa dawa Makwati ili akupende wewe zaidi ya mwingine.”

Makwati alikuwa na wake wanne ambao walioishi katika maisha ya uhasama sana. Walitukanana na kusingizia mambo mabaya kama uchawi. Kimsingi, penzi haligawiki. Wanajamii wanapaswa kuachana na mila hiyo mbaya ya kuishi katika ndoa inayohusisha mke zaidi mmoja.

  1. Dhana potofu

edu.uptymez.com

Katika jamii kumekuwa na hali ya watu kuamini vitu ambavyo havina msingi. Watu wamekuwa wakitelekeza walemavu wa viungo vya mwili, Zeruzeru na hata mapacha kwa kuamini kuwa miungu yao isingefurahia kuwaona watoto hao wenye ulemavu katika jamii. Mwandishi wa riwaya hii hakufumbia macho tatizo hili, amelizungumzia  kwa kina na kuwaonyesha njia kuwa mambo ambayo walidhani kuwa yamewezekana. Ziki ni mfano wa watu ambao wamekuwa na dhana potofu maishani mwao. Sekai na Takadini (Zeruzeru) wanapokaribishwa katika kijiji cha watu wa Masasa, Ziki alipinga kuwepo kwao hapo. Anasema,

        “Sote tunajua mila za mababu zetu katika kila koo na kijiji. Watoto kama huyu lazima wauawe, wenye ulemavu lazima wauawe, na hata pacha mmoja lazima auawe”.

Hii ni kauli ya Ziki ambayee alirejea mila na desturi potofu kuhalalisha dhana potofu alizonazo dhidi ya walemavu. Huyu si mtu ambaye ana dhana potofu, wapo wengi sana. Katika riwaya hii, wapo wazee wengine kama Mapunzure ambaye katika ukurasa 35 alisisitiza, Mtoto lazima auawe.”Pia kama mzee Manyamombe ni mmoja wa watu wenye imani potofu juu ya watoto walemavu.

Kuna dhana potofu pia kuhusu jinsia ya watoto. Wazazi wengi wamekuwa na upendeleo zaidi kwa watoto wa kiume kama ilivyo kwa Makwata na wake zake.

                  Sekai anapopata ujauzito anatamani mumewe kuwa huenda ujauzito alionao ni wa mtoto wa kike. Makwati aling’aka,

        “unasemaje we mwanamke?… Hapa tayari tuna idadi kubwa ya wanawake. Mimi nanyong’onyea kwa kuomba mtoto wa kiume.”

Kila mtoto anayezaliwa ana haki ya kupendwa bila kujali jinsia yake.

Dhana potofu katika ni tatizo linalopaswa kuondolewa kwa kutoa elimu sahihi katika jamii ili kuepuka matatizo yasitokee kama mzee Chivero na mtemi Masasa walivyofanya kwa watu wao.

  1. Nafasi ya mwanamke katika jamii na ujinsia

edu.uptymez.com

Ujinsia ni majukumu ya kijamii ambayo hupewa mwanaume au mwanamke kwa kuangalia mahusiano ya mtu mume na mtu mke. Ni wajibu wa mume na mke katika jamii.

                Katika jamii nyingi kiafrika kumekuwa na matatizo ya jinsia kama vile kuozesha kuwa watoto katika umri mdogo na kulazimishwa kuolewa au bila ridhaa, maamuzi yote yanayohusu jamii na familia hufanywa na wanaume, watoto wa kike wamekuwa hawapewi thamani sawa na watoto wa kiume na suala zima la malezi amekuwa akiachiwa mama peke yake.

             Katika riwaya hii, mwandishi ameonesha matatizo ya kijinsia. Kwa mfano, Tendai alilzaimshwa kuolewa na mtemi Masasa na alikuwa na umri mdogo. Sekai anapomuuliza Tendai kama alimpenda mzee Masasa, Tendai alijibu,

             “Ni heshima kuwa mke wa mtemi mwenye nguvu kama Masasa. Lakini namchukulia kama baba yangu kuliko mume wangu”…(uk.47)

Kauli hii inathibitisha kuwa Tendai hakufurahia kuolewa na mume mwenye umri mkubwa sawa na baba yake. Hii ni kasoro kubwa sana katika suala zima la ndoa. Tendai anaendelea kusema,

            “Wake wenzangu ni kama mama zangu. Siku zote wananitazama mimi, wananikaripia, na mabinti zao ambao ni wa umri wangu hunicheka kwa dharau kila wanitazamapo…” (uk.47)

Mahusisano ya kijinsia katika jamii yamekuwa katika hali ya kukandamiza zaidi, mwanamke na kumpendelea mwanaume. Katika riwaya hii, mwandishi ametuonyesha tatizo jingine la kijinsia kuwa ndoa za mitala. Katika suala zima la ndoa mitala tunaona mwanaume anapewa fursa ya kuoa mke zaidi ya mmoja. Fursa hiyo haionekani kwa mwanamke. Sababu kubwa inaonekana kuwa mwanamke ni kama chombo cha starehe. Kwa mfano Makwati alikuwa na wake wa nne. Mtemi Masasa alikuwa na wake wengi pia. Hapa mwanaume ndiye mwenye nguvu zaidi.

                Kuhusu nafasi ya mwanamke mwandishi amemuonyesha mwanamke kama mzazi na mlezi wa watoto na familia kwa ujumla. Kwa mfano, Sekai ni mama mzazi wa Takadini. Alimlea na kumlinda wakati wote mpaka alipopata mke (Shingai). Mashangai alimzaa Shingai na kumlea wakati wote. Kazi ya kulea ilionekana ni ya mwanamke na si mwanaume. Mashangai anasema,

           “Shingai sitakuita mwanangu tena, umefanya kitu gani hiki? Hivi ndivyo bibi yako na tete wako walivyokufundisha?…(uk118).

Kauli ya mama mzazi wa Shingai inathibitisha kuwa malezi ya mtoto waliachiwa akina mama, mama wazazi, Shangazi na bibi. Haya si mawazo ya wanawake kuona ni jukumu lao tu, pia hata wanaume walikuwa na dhana hiyo hiyo. Mfano, Baba yake Shingai alimhoji kewe kuhusu malezi ya Shingai kwa kusema,

                “Hukumfundisha mwanao maana ya tendo hilo, we?…(uk96)

Mwanake amechorwa pia kama mwanamapinduzi. Haya yanaweza kuthibitishwa na wanawake wawili ambao ni Sekai na Shingai. Ni wanawake walioleta mabadiliko katika jamii kwa mfano, Sekai na mwanamke wa kwanza kuvunja sheria za mila na desturi za jamii yake kwa kukataa Takadini(Zeruzeru) asiuawe na akamlinda wakati wote.na alileta mapinduzi akiwa uhamishoni. Rafiki yake Tundai anasema,

          “Kwa sasa ,sifikiri kwamba kuna mtu yeyote atakayekuwa na moyo wa kuharibu watoto wachanga, Masope au wenye ulemavu…”

Shinga naye anaonekana ni mwanamapinduzi kwa kukataa kuchaguliwa mtu wa kumwoa. Aliamaini kuwa ndoa ya kweli inahusisha watu wawili waliopendana na ambao wamechaguana. Shingai anasema.

             “Amai, siyo kama ninamchukia Nhamo la hasha. Isipokuwa sidhani kama nitakuwa na furaha kuishi naye”(uk.110)

Anaendela kusema,

             “Huyu ndiye mtu ninayetaka anioe. Hakuna aliyeniuliza kama nampenda Nhamo… lakini katu kwa Nhamo siendi hata kama angekuwa name sasa”…118

Shingai alisimamia msimamo wake na hata akaamua kuolewa na Takadini na kupata mtoto ambaye hakuwa Sope.

Kwa ujumla, matatizo ya kijinsia yanachangiwa sana na athari za utamaduni (mila na desturi) katika mfumo wa maisha ya jamii. Jamii kuongozwa kwa mfumo unaoegemea jinsia moja ndiyo chanzo cha ukandamizaji wa kijinsia. Jamii zinazofuata mfumo dume, huwa na mila zinazokandamiza wanawake zaidi. Ukombozi wa kiutamaduni utaleta usawa wa kijinsia katika jamii.

  1. Umoja na mshikamano

edu.uptymez.com

Umoja ni ile hali ya kuwa pamoja : ushirikiano na mshikamano ni ile hali ya watu kuwa na msimamo na ushirikaino wa karibu katika kutimiza azima Fulani.

          Mwandishi wa riwaya hii ameonesha mbinu mojawapo katika kupambana na mila na desturi potofu ni kwa jamii kuwa na umoja na mshikamano. Umoja na mshikamano ni silaha katika mapambano haya. Mshikamano mzuri alionesha mzee Chivero, Tendai, mtemi Masasa ulisaidia kumlinda Takadini dhidi ya wanyanyapaa na hatari ya kupoteza maisha. umoja na mshikamano uliendelea kukua zaidi pale Shingai alipoamua naye kuonesha msimao kwa kukataa kufuatia mila na desturi zilizowabagua walemavu, kuwalazimisha wanawake kuolewa kwa nguvu na hivyo kuamua kuolewa na Takadini ambaye alikuwa ni mlemavu wa mguu na pia alikuwa zeruzeru.

Katika hali ya ushindi dhidi ya mila potofu, mzee Makuru anasema,

           “Nilimwambia hivyo….. Sasa tunajua ni kipi ambacho mizimu yetu haikuruhusu kutafuta, Sope hawezi kuzaa Sope! Naamini tutajifunza somo hili, fuvu la nyani limekuwa kijiko kwa mlo wa mahindi: vizazi vijavyo vitatushukuru kwa kile tulichokifanya hapa kijijini.”

Katika mapambano yote yote yale, umoja na mshikamano husaidia sana katika kupata ushindi. Wahenga walisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Umoja na mshikamano wa Shingai, Pindai, Chivero, Masasa, Sekai Takadini, Makaru na Tendai ulisaidia kuleta mabadiliko makubwa ya kiutamaduni katika jamii yao.

  1. Ujasiri

edu.uptymez.com

Hii ni hali ya kukabili jambo bila ya hofu, uhodari, ushujaaa. Katika riwaya hii ya Takadini mwandishi ameonesha ujasiri kama mbinu muhimu katika ukombozi wa kiutamaduni. Pengine ujasiri siyo mbinu inayotumika katika ukombozi wa kiutamaduni tu, bali ni mbinu ambayo imetumika katika aina zote za ukombozi. Mathalani katika riwaya hii tunakutana na Sekai, mwanamke anayeamua kupambana na mila na desturi ambazo ziliwakandamiza wanawake. Baada ya kumzaa Takadini aliamua kumtorosha mwanawe ili asiuawe. Alimkabili mumewe kuwa alitaka kumuona mwanawe akiwa hai. Na hata anapokuwa uhamishoni.

              Shingai ni mwanamke mwingine ambaye alionesha ujasiri mkubwa katika harakati za kujikomboa katika makucha ya mila na desturi zilizokuwa zikiwakandamiza wanawake na watoto. Shingai aliamua kuolewa na Takadini (Kijana mlemavu) na kupuuza uchaguzi wa wazazi wake kwa kuwa aolewe na Nhamo. Kwa ujasiri kabisa Shingai anasema,

                  “Huyu ndiye mtu ninayetaka anioe. Hakuna aliyeniuliza kama nampenda Nhamo. Wewe na baba mlikuwa na hamu ya kuniozesha katika familia ya Manyamombe hata matakwa yangu hayakusikilizwa…. Sasa nimechagua.”

Shingai aliendelea nma ujasiri wake huohuo hat baada ya baba yake kutoa kauli za kumkana kuwa mwanae kwa sababu ya kuolewa na Sope (zeruzeru).

Ujasiri ni nguzo muhimu sana katika mapambano dhidi ya mila na desturi potofu katika jamii. Ni lazima tuondoe hofu na woga ili tubadili hali ya ukandamizaji na uonevu ndani ya jamii kwa kunyoshea vidole mila mbaya. Kwa ujumla, malezi ya waatoto ni jukumu la wazazi wote. Mtoto ambaye helelewa vyema na baba na mama ndiye huwa na tabia bora. Jamii inapaswa kutambua kuwa malezi ya baba na mama ni haki ya mtoto, mila ambazo haziendaini na malexi bora hatuna budi kuachana naazo.

  1. Malezi ya watoto

edu.uptymez.com

Malezi ni makuzi ya watoto. Ni njia watumiayo wazazi katika ukuzaji wa mtoto kwa kutarajia kufuata tabia na mwenendo unaostahiki.

       Malezi ya watoto yanapaswa kusimamiwa na wazazi wote wawili. Baba na mama wanapaswa kushirikiana kwa pamoja katika kulea watoto wote ili watoto wawe na tabia njema. Mila na desturi katika jamii zinazofuata mfumo dume zinakuwa zikaachwa wanawake peke yao kuwa ndiyo walezi wa watoto. Wanawake ndiyo wanawajibika na malezi ya watoto kwa wanaume zao. Mfano mzuri tunaweza kuupata katika riwaya hii ya Takadini.

Malezi anayopa Shingai ni mama, bibi na shangazi. Baba yake Shingai mzee Nhariswa anamwajibisha mkewe kwa kumpiga kwa sababu Shingai anaonekana kutofuata mila na desturi katika ukurasa wa 119 mzee Nhariswa ansema

          “umefanya nini sasa wewe mwanamke? Tangu mwanao alipopeleka maji kwa Sekai ungefuatilia kujua anachokifanya …. Uliona dalili, kwa nini hukutafuta dawa…”

Mwandishi anasema kuwa Nhariswa alimpiga mkewe kichwani na usoni mara kadhaa, lakini mkewe hakuweza kujibu. Kitendo hiki kinadhihirisha walakini wa baadhi ya mila na desturi kuhusu suala zima la malezi katika kajamii.

    “Hivi ndiyo bibi yako na tete wako walivyokufundisha?” (uk118)

Mama huyu naye anaona malezi ya watoto yapo mikononi mwa wanawake na si jukumu la wazazi wote.

     “….Mume wangu unasemaje? Kama mtoto wetu ni sope, nitahuzunika sana, lakini nina uhakika atampata wa kumpenda kama nilivyokupenda wewe. Acha kuwa na shaka nimembema mimi na ninaelewa atakuwa kama watoto wengine. Njoo mume wangu tulale sasa.”

Mapenzi ya dhati ni muhimu sana katika ukombozi wowote ule katika jamii.ukombozi wa kitamaduni unawezekana kama kweli watu watakua na mapenzi ya dhati.

Ujumbe

Mwandishi wa riwaya hii anatoa ujumbe ufuatao kwa jamii:

  1. Walemavu wana haki ya kuishi sawa na watu wasio kuwa na walemavu.
  2. Malezi ya watoto yanapaswa kuwa kusimamiwa na wazazi wote wawili ili kujenga jamii inayoheshimika.
  3. Ndoa ni maamuzi ya watu wawili wapendanao na hayapaswi kuingiliwa na mtu yeyote.
  4. Ujasiri, umoja na mshikamano ni mbinu muhimu sana katika ukombozi wa kiutamaduni.
  5. Jamii inapaswa kuachana na mila na desturi potofu ili kuondoa ukandamizaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu.

edu.uptymez.com

Mtazamo wa Mwandishi

Mwandishi wa riwaya ya Takadini anaoneka kuwa na mtazamo wa kiyakinifu.

Mwandishi anachukulia matatizo yanayotokana na mila na desturi kuwa yanaweza kutatuliwa na watu wenyewe kwa kuchukua hatua za makusudi kabisa katika kujikomboa kiutamadunio kama anavyofanya Sekai, Shingai, Masasa na mzee Chivero. Mwandishi ameweza kuonyesha waziwazi matatizo hayo ya kiutamaduni kuwa ni ukandamizaji wa kijinsia, uonevu kwa walemavu, n.k. Mwandishi pia ameonesha njia za kujokomboa kiutamaduni kuwa ni umoja, mshikamano, elimu na ujasiri.

            Kwa ujumla mwandishi ameainisha matatizo yote ya kiutamaduni na kuweza kuonesha masuluhisho ya matatizo haya, hivyo mwandishi anamtazamo wa kiyakinifu.

Msimamo wa mwandishi

Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi kwani ameeleza udhaifu wa baadhi ya mila na desturi zetu. Mwandishi ameonesha madhara ya kuendela kukumbatia  mila hizo na akaonyesha hoja ya kufanaya mabadiliko ya badhii ya mila hizo ili kuleta uhuru, haki, usawa na kutahmini utu wa watu wote.

Falsafa ya Mwandishi

Mwandishi anaelekea kuamini kuwa binadamu wote ni sawa hata kama kuna tofauti za kimaumbile. Kila binadamu ana haki ya kuishi. Kwa ujumla mwandishi ni muumini wa haki na usawa.

Migogoro

Katika riwaya hii kumejitokeza migogoro mingi ambayo imetokana na mgogoro wa kiutamaduni.

Mgogoro wa kwanza: Mgogoro wa kiutamaduni kati ya Mkwati na Sekai. Mgogoro huu ulizuka mara bada ya Sekei kuzaa mtoto ambaye ni Sope (Zeruzeru). Kutokana na mila na desturi, mtoto ana ulemavu wowote ule alipaswa kuuawa hivyo Takadini alipaswa kuuawa siku ileile aliyozaliwa. Suala la kuuawa kwa Takadini hakuliafiki Sekai na hivyo kulipinga kwa nguvu zote.

              Suluhisho la mgogoro huu ni kwamba Sekai alitoroka na kuishi uhamishoni hadi Takadini alipokua na kuoa na kupata mtoto wa kiume ambaye si sope ndipo aliporudi kijijini kwao.

Mgogoro wa pili : Ni kati ya Shingai na wazazi wake. Wazazi wa Shingai walimchagulia mume wa kumuoa Shingai. Kijana aliyependekezwa aliitwa Nhamo. Jambo hili halikumfurahisha Shingai hivyo alikataa kuolewa na Nhamo na hivyo kufanya wazazi wake kukasirishwa sana kiasi cha kumueleza kuwa asiwatambue kama ni wazazi wake.

             Suluhisho la mgogoro huu ni kwamba Shingai aliamua kutorokea kwa Takadini (kijana aliyempenda sana) na kuolewa na Takadini.

Mgogoro wa tatu: Ni wa kinafsia ambao unajitokeza kwa Tendai. Tendai aliozwa kwa mzee Masasa ambaye alikuwa na umri wa baba yake na wakewenza walikuwa umri wa mama yake na mabinti wa Mtemi Masasa walikuwa umri sawa na Tendai. Tendai alishindwa amuite mume wake au baba yake, alishindwa awaite wake wenza au mama zake. Hakuwa amani moyoni. Alikuwa katika hali ya upweke mno.

            Suluhisho la mgogoro huu ni kumtafuta rafiki ambaye ni Sekai ili wasaidiane mambo mbalimbali.

Mgogoro wa nne: Ni mgogoro wa kijamii. Mgogoro huu ulitokea kati ya Shingai na Chido. Mgogoro huu ulimhusisha Nhamo kwani Chido alidhani Shingai atolewa na Nhamo na kumfanya awe mkemwenza. Mgogoro ulifanya wanawake hawa wawili watupiane maneno au vijembe.

                Mgogoro huu ulisuluhishwa kwa Shingai kueleza msimamo wake wa kutomtaka Nhamo awe mme wake.

                 Pia Shingai alipoolewa na kuzaa na Takadini ilisaidia kupunguza uhasama huo.

Mgogoro mwingine ni wa kijamii: Huu ni mgogoro wa tano ambao unahusisha Takadini na Nhamo. Nhamo alikuwa ni mgomvi, mbaguzi jambo ambalo alilifanya kwa Takadini. Uhasama zaidi uliongezeka pale Shingai alionesha mapenzi Kwa Takadini Na kumkataa Nhamo. Hakuna suluhisho linalotolewa katika mgogoro huu.

FANI

  1. Muundo

edu.uptymez.com

Katika riwaya hii ya Takadini mwandishi ametumia muundo wa msago (moja kwa moja). Visa na matukio katika riwaya hii vilipangwa kwa mfululizo wa moja kwa moja na kazi nzima ina jumla ya sura kumi na tatu. Kwa ujumla muundo wa riwaya hii ni wa moja kwa moja kwani mwandishi anatuonesha namna Sekai alivyopata mimba, akazaa mtoto wa kiume ambaye ni sope(Zeruzeru), kisha anatoroka kwenda kuishi, uhamishoni, maisha ya Sekai uhamishoni, Takadini anakua na kupata mke aitwae Shingai na mwisho tunaona kijijini kwao.

  1. Mtindo

edu.uptymez.com

Mwandishi ametumia mtindo wa masimulizi katika riwaya yake. Sehemu kubwa mwandishi amehadidhia mwenyewe kuhusu maisha ya Sekai na Takadini.

                 Vile vile kuna matumzi ya dayolojia katika sehemu chache. Mwandishi ametumia dayolojia kuonesha uahalisi wa kauli za wahusika wake. Mfano Dayolojia imetumika katika (uk.1)

         “Je, Na yule mbuzi wako uliopewa Na baba Makwati, amekupatia watoto wangapi?”

         “Tangu nimpate ni miaka miwili tu na tayari ana watoto wawili nabado anatarajia mwingine“.

Haya ni majibizano kaati ya Dirai na Rumbidzai.

 Nafasi zote tatu zimetumika. Nafasi ya tatu umoja ndiyo imetalawa katika sehemu kubwa ya riwaya. Kwa mfano:

  • Nafasi ya I ——- “Ndiyo, Pindai, anaogopa……” – (uk.3)
  • Nafasi ya II —–   “Unasemaje wewe mwanamke?”’ (uk.4)
  • Nafasi ya III —— “Sekai alipofumbua macho yake……” (uk.5)

edu.uptymez.com

 Kuna matumizi ya tanzu nyingine ndani ya riwaya. Mwandishi ametumia nyimbo. Kaatika ukurasa wa pili Rumbidzai aliimba,

 “Mashamba yote yamelimwa

 Mbegu nazo zimepandwa

 Zimechipua na kumea,

 Sisi watatu tumepata mavuno yetu;

 Mheshimiwa wetu amemiliki mavuno

 Kwa mikono yake halisi

 Kutoka mashamba yetu yote

 Lakini ni kipi alichoambulia

 Kutoka ardhi ile isiyomea kitu?…”

Nyimbo nyingine zinajitokeza (uk34, 57, na 90)

 Matumizi ya monolojia yamejitokeza pia katika riwaya hii:   Mfano wa monolojia:

 “Hatimaye!” Sekai alijinong’oneza peke yake.

 “Mababu zangu wamenitimizia ombi langu kuu. Sasa wake wenzangu wataniheshimu kama mke wa kwanza. Hata wakwe zangu watakoma kumwambai mume wangu anirejeshe kwetu. Nina hakika ya kijifungua mtotot wa kiume….” (uk1)

 Mwandishi pia ametumia mbinu ya hadithi ndani ya riwaya. Mbinu hii imejitokeza katika uk. 82 -84. Kwa ujumla, mwandishi amesheheneza mbinu mbalimbali za kimtindo katika kazi yake.

 Matumizi ya Lugha

 Lugha iliyotumika inaeleweka kwa wasomaji kuwa wengi. Mwandishi ametumia tamathali za semi, misemo na mbinu nyingine za kisanaa.

 a)     Misemo na Nahau

 Katika riwaya hii kuna matumizi ya misemo na nahau mbalimbali. Misemo na nahau zimetumia kupamba lugha na pia kuonesha uzito wa ujumbe uliokusudiwa.

 Kwa mfano:

 “Lakini mbwa huyu amepoteza meno yake yote”. (uk31).

 Hii ni nahau zenye maana ya mtu kutoakuwa rijali tena. Mifano ya misemo  ni:

 Habari njema huchechemea kwa mguu mmoja, lakini mbaya hukimbia kama sungura.” (uk.15).

 Msemo huu una maana ya kuwa habari nzuri hazienei haraka lakini zile mbaya huenea haraka sana. Mifano mingine ya misemo ni:

 “Pokea upewacho”…(uk10)

 “…Maisha ni matamu”..(uk83)

 “Kanga hawezi kutua juu ya bua la mtama…..(101).

 “Mume ni kiungo kwa mwanamke.”.(110).

 b)    Tamathali za Semi

 Tashibihi:

 Mwandishi ameweza kulinganisha vitu kwa kutumia vuinganishi kama vile: kama,mfano wa, sawa na, nk

 Kwa mfano:

  • Giza jepesi tu lilibaki ukutani  kama mgeni asiyekaribishwa na asiyetaka kuondoka.(uk…5).
  • Muda huenda polepole sana mithili ya mwendo wa kakakuona. (uk. 6)
  • Mwanzo maumivu hayo yalitulizana sawa na mwisho wa sentensi ndefu. (uk.6).
  • Mtoto alionekana mweupe sana na funza mkubwa (uk. 16)

edu.uptymez.com

Tashihisi                                 

 katika riwaya hii ya Takadini mwandishi amevipatia vitu sifa walizonazo watu.  Kwa mfano:

  • Ndege mbalilmbali wakiimba kukaribisha siku mpya. (uk. 5)
  • Ubongo wake ulioathirika kwa mawazo uliufukuza usingizi. (uk. 17)
  • Fikra zilizopingana zilijichomeka katika nafsi yake(uk. 17)
  • Miaka mingi iliyomchakaza iliufanya uso uwe sawa na mlima uliomomonyoka ardhi. (uk… 20)

edu.uptymez.com

Mubaalagha:

 Kuna hali ya utiaji chumvi au chuku nyingi katika masimulizi ndani ya riwaya ya Takadini.

 “Mtemi Masasa na wenzake walimtazama Sekai, mcho yao yakipiga mahesabu. Kila mmoja aliridhika naye – tangu monifu nyuma ya miguu yake, mapaja yaliyojaa na hata  matiti  yake ya duara yaliyojaa maziwa”.(uk.37).

 Je, ni kweli wanaume wote waliokuwepo walipiga mahesabu sawa kuhusu Sekai? Mwandishi ametia chumvi kuonesha mvuto tu wa Sekai.

 Ritifaa:

Tamathali hii imetumiwa na baadhi ya wahusika kwa kuzungumza nakitu au mtu ambaye husikika katika fikra.

Kwa mfano: Sekai anasoma;

“Hatimaye! Mababu zangu wamenitimizia ombi langu kuu….”(uk.1).

pia katika ukurasa wa 107 manyamombe anasema,

“…Njoo,mpendwa Chivero,umezurura milimani na msituni kwa muda mrefu…

Tusamehe kwa kukuacha mbalimbali …. Njoo rejea nyumbani…. Kunywa pombe hii ….”

Wahusika wote wawili ( Sekai na Manyamombe) walizungumza na watu ambao hawaonekani. Mbinu hii ndiyo tunayoiita Ritifaa.

Dhihaka

Kuna matumzi ya tamathali zenye kunesha dharau na yenye lengo la kumweka mtu katika hali duni kupita kiasi, lakini kwa mbinu ya mafumbo.

Kwa mfano:

  • Naamini alichobeba ni mtoto halisi, siyo dubwasha.” Haya maneno yalimlenga Sekai kwa kuwa siku zote waliamini hazai.(uk.2).
  • Ha! Yawezekana hana tatizo lolote lile, labda alikunywa maziwa mengi wakati wa ujauzito….”

edu.uptymez.com

Kauli hii ilitolewa kwa Sekai baada ya kubaini kuwa amezaa mtoto Sope.

Tafsida:

Mwandishi kwa kiasi kikubwa amezingatia utamaduni wa lugha ya Kiswahili. Ameweza kutumia maneno ambayo yanaficha ukali wa maneno. Hakutumia lugha ya matusi. Kwa mfano:

  • Akamshambaulia hata sehemu zake za siri. (uk.83)
  • “A kajivuta karibu zaidi naye, chini ya gudza. Hawakuzungumza, wakafanya kile ambacho kilitokea kwa asili ya maumbile. Wakakata kiu ya hisia zilizowavuta pamoja miezi mingi”. (uk.117)
  • “Walifanya tena tendo la ndoa, …”(uk. 117)

edu.uptymez.com

c)     Mbinu nyingine za kisanaa

i)        Takriri: Kuna baadhi ya silabi, maneno na sentensi zimejirudia kwa lengo la kuonesha msisistizo.

Kwa mfano takriri imejitokeza katika (uk.62)

Pale Nhamo anaposema,

  • Wewe ni Sope, sope, sope”
  • “Najua, najaua” (uk.79)

edu.uptymez.com

ii)       Mdokezo:

Kuna hali ya kutatiza maneno bila kukamilisha sentensi katika riwaya hii.

Kwa mfano:

  • “Siku moja sijui lini …. Lakini hivi” (uk.75)
  • “Sukuma mara moja tena…” (uk.125)
  • Mtu mzima kama watu wengine na amea…..?

edu.uptymez.com

Nidaa:

Kuna kauli ambazo zinaonyesha kushangazwa kwa jambo Fulani. Kwa mfano:

“Ah, Ha! – (uk.118)

“Kumbe maisha ni matamu!” (uk83)

Tashititi:

Hi ni mbinu ya kuuliza swali kwa jambo ambalo anafahamu jibu lake.

Kwa mfano:

“Huenda atakuwa wa kike”. Sekai alisema bila dhamira kubwa.

“Unasemaje we mwanamke? Makwati aliongea kwa sauti kali.

Swali analouliza makwati tayari jibu lake analo.

Wahusika

       A.Takadini

  • Huyu ndiye mhusika mkuu wa riwaya hii.
  • Ni mtoto wa kwanza wa Sekai.
  • Ni mlemavu wa ngozi (Zeruzeru) na ana tatizo la mguu.

edu.uptymez.com

Kijana wa kiume.    

  • Ni mchapakazi na mtu anayependa kujifunza.
  • Ni mwenye huruma.
  • Ni mtiifu.
  • Ni jasiri.
  • Ni mwanamapinduzi.
  • Ni mhanga wa mila na desturi mbaya zinazobagua walemavu.
  • Anafaa kuigwa na jamii.

edu.uptymez.com

          B:Sekai

  • Huyu ni mhusika mkuu mwingine.
  • Ni mke wa kwanza wa Makwati.
  • Ni mwanake mchapakazi.
  • Ni mhanga wa mila na desturi zilizopitwa na wakti.
  • Ni mwanamapinduzi.
  • Ni mama mzazi wa Takadini.
  • Ni jasiri.
  • Ni mwenye huruma.
  • Ni mwenye busara.
  • Ni mvumilivu.
  • Ni mnynyekevu.
  • Ni mchapakazi.
  • Ni mpole.
  • Ni mama mzazi na mlezi mzuri wa familia
  • Ni mama mwenye upendo.
  • Ni mpishi mzuri wa chakula.
  • Anafaa kuigwa na jamii

edu.uptymez.com

 C: Makwati
Anafaa kuigwa na jamii.
Ni mkale.
Ni mwoga.
Ana upendo kwa mkewe.
Ni mume mwenye wake wanne.
Ni baba mzazi wa Takadini.
Ni mume wa Sekai.

 D:Chivero

  • Ni mzee wa makamo.
  • Ni mganga wa kienyeji.
  • Alikuwa mpiganaji katika vita.
  • Mtu mwenye upendo.
  • Ni mtu mwenye busara.
  • Ni mshauri mkuu wa mtemi Masasa.
  • Mpenda mabadiliko.
  • Ana huruma.
  • Ni mfanyakazi shupavu.
  • Ni mzalendo.
  • Ndiye aliyewapokea Sekai na Takadini.
  • Anafaa kuigwa na jamii

edu.uptymez.com

 E:Mtemi Masasa

  • Ni mzee wa makamo.
  • Ni mtemi wa kijiji cha watu wa Masasa.
  • Ni mpole.
  • Ni mcheshi.
  • Ni mzee mwenye hekima
  • Ana wake wengi.
  • Ni mpiganaji wa vita.
  • Ni mfugaji.
  • Anafaa kuigwa jamii

edu.uptymez.com

       F:Shingai

  • Anafaa kuigwa na jamii.
  • Ni jasiri.
  • Ni msichana mwenye msimamo.
  • Ni jasiri.
  • Ni mwanamapinduzi.
  • Ni mke wa Takadini.
  • Ni binti wa mzee Nheriswa.
    G: Tendai
  • Ni mpole.
  • Ni mwanamapinduzi.
  • Ana upendo.
  • Ni mkarimu.
  • Ni mke mdogo wa mtemi Masasa.
  • H:Darai
  • Ni mke wa tatu wa Makwati.
  • Ni mtu makali.
  • Ni mpenda majungu.
  • Ana wivu.
  • Mbinafsi.
  • Ni mama wa Chipo
  • Ana mawazo potofu
  • Ni mnafiki.
  • Hafai kuigwa na jamii.
  • I:Rumbidzai
  • Ni mke wan ne na mdogo kabisa wa Makwati.
  • Ni mtu mkali.
  • Ni mpenda majungu.
  • Ana wivu.
  • Mbinafsi.
  • Ana mawazo potofu.
  • Hafai kugwa na jamii

edu.uptymez.com

   J:Manyamombe, Mukaru, Chimbiri, Makaure

  • Hawa ni wazee kwa umri.
  • Ni wazee wa baraza la mtemi Masasa.
  • Ni wasimamizi wa mila na desturi za kabila lao.
  • Ni wapiganaji wa vita.

edu.uptymez.com

Wahusika wengine:

–         Nhamo

–         Maishingai
–          Pindai

–         Ambuya Tungai

–         Ambupa Shungu

–         Pedeisai

–         Mtemi Zvedi

–         Tupfumaneyi

–         Chengatai

–         Chido

–         Ambuya Rekai

–         Mtemi Chinjeyari

Mandhari

Riwaya hii ya Takadini imetumia ya vijijini katika nchi ya Zimbabwe katika karne ya 19. Katika masimulizi haya ya riwaya mandhari yake inaweza kugusa vijiji vya nchi nyingi za Kiafrika ambazo zipo katika dunia ya tatu. (Nchi zilizoendelea)

Jina la Kitabu

Jina la kitabu ni Takadini. Ni jina ambalo linatoka na jina la mhusika mkuu anayeitwa Takadini. Jina hili pia alipewa na mama yake aliyeitwa Sekai. Jina la Takadini lina maana ya “Sisi tumefanya nini”‘?

Jina la kitabu linasanifu yaliyomo katika kitabu hiki kwani kwa kiasi Fulani jina hili linajumuisha mambo yaliyotokea wakati wa uzazi wa mtoto Takadini na matatizo yote waliyokumbana nayo yanayotokana na mila na desturi zinazowabagua watoto na wazazi wa watoto ambao ni Zeruzeru. Takadini yaani “Sisi tumefanya nini?” Linaakisi vilio vya walemavu wote ambao wanatengwa na kuuawa kwa Baraka za wazee wanaosimamia mila hizo. Hawakupenda kuzaliwa viwete, zeruzeru, vipofu na viziwi. Wazazi wao pia hawakupenda iwe hivyo. Kama ndivyo kwa nini kuna adhabu kama hizo? Kwani wamefanya nini? Muumbaji na Mungu na Mungu hana makosa katika uumbaji wake.

Kwa ujumla jinala kitabu linasadifu yaliyomo ndani ya kitabu kwa kuangalia maisha ya mhusika mkuu na matatizo anayopata yanamfanya mhanga yeyote wa mila mbaya aulize swali hili muhimu la SISI TUMEFANYA NINI? Na maana ya swali hili ndilo linatupatia jina la TAKADINI.

KUFAULU NA KUTOFAULU

Kufaulu Kimaudhui

Mwandishi amefaulu kwa kuweza kuonesha matatizo wanayopata watu wenye ulemavu. Mwandishi pia ameweza kuainisha tatizo kubwa linalichangia walemavu kutokubalika ndani ya jamii kuwa ni mila na desturi ambazo zinapandikiza dhana potofu kuhusu walemavu.

     Mwandishi pia hakuishia kubainisha matatizo tu, pia ametoa masuluhisho ya matatizo hayo kuwa ni elimu, ujasiri, kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati.

Kufaulu Kifani

Mwandishi wa riwaya hii amefaulu sana kuonesha ufundi wake katika kusuka kazi yake. Ametumia lugha rahisi ya kueleweka lakini yenye tamathali za semi za kutosha na kuna matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa. Vilevile ameweza kuhusu visa na matukio kwa muundo wa moja kwa moja ili kuwapatia wasomaji urahisi wa kufuatilia kwa umakini matukio yote.

    Mwandishi pia ameonesha kupevuka sana katika kipengele kizima cha mtindo. Ameweza kutumia nafasi zote,             matumizi ya tanzu nyingine kama vile nyimbo na hadidhi ndani ya riwaya.

Amefaulu pia kuteua jina la kitabu ambalo linabeba jina la mhusika na maudhui yaliyomo ndani ya kitabu.

 Kutofaulu

Kimaudhui mwandishi ameshindwa kuhusisha walemavu wengine katika kilio cha Takadini yaani tumefanya nini? Mwandishi ameonesha Zeruzeru tu. Angeweza kuonesha matatizo ya mila na desturi yanavyoathiri walemavu wengine.

  Kifani mwandishi ametumia idadi ya wahusika bila sababu ya msingi. Idadi kubwa ya wahusika inatakiwa kuwa kielelezo cha upana wa maudhui yaliyomo ndani ya kitabu. Mwandishi pia ameshindwa kuonesha wanakijiji na watu wa kijiji cha asili cha Sekai walipokeaje hali ya takadini kwa kuoa mtu ambaye si mlemavu na kuweza kuzaa mtoto ambaye hakuwa na ulemavu ili liwe funzo kwa jamii zote.

Share this post on: