Form 3 Kiswahili – VITABU TEULE VYA FASIHI

Share this post on:

                                UHAKIKI WA TAMTHILIYA

Jina la kitabu  – Ngoswe- Penzi kitovu cha Uzembe

Mwandishi        – E. SEMZABA

Mchapishaji   – Nyambari Nyangwine Publishers, 2006


Utangulizi

Wasanii kama sehemu ya jamii wanapaswa kushirikiana kikamilifu katika mipango ya kitaifa. Mipango mingi inahusishwa na mipango mingine ya kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni. Ili mipango hii iweze kukamilika, suala la kujua idadi ya watu ni la msingi.

Ngoswe ni tamthiliya inayoangalia kwa makini suala la uhesabuji wa watu na utayari wa watu wenyewe kuhesabiwa. Aidha tamthiliya inaonyesha hali na wajibu wa watu wanaokabidhiwa dhamana ya kupanga kazi ya kuhesabu watu.

Maudhui

Ngoswe – Penzi Kitovu cha Uzembe ina dhamira mbalimbali zinazojitokeza:

Suala la mapenzi

Tamthiliya ya Ngoswe – Penzi Kitovu cha Uzembe inaliweka suala la mapenzi kuwa “kitovu” kikubwa cha uzembe. Katika kufafanua na kuthibitisha hoja au dhamira hii mwandishi anawatumia Ngoswe na Mazoea. Ngoswe kama kijana wa kiume na ofisa mhesabuji wa watu, anaonekana kuwa na uchu wa mapenzi mara anapomwona Mazoea (uk 5).

Kitendo cha “kupenda” si kibaya kwani ni sehemu ya maisha ya binadamu lakini jambo la msingi kuelewa hapa ni “jinsi na namna ya kupenda”Tatizo kubwa linalojitokeza katika tamthiliya hii kile kinachomfanya afisa Ngoswe kupenda kiasi cha kuharibu kazi. Ngoswe hawezi kulaumiwa kwa kumpenda Mazoea, ila analaumiwa kupenda bila kujizuia na kufika hatua ya kumtorosha Mazoea (uk 24-28). Katika mapenzi yanayoonyeshwa na Ngoswe. Athari zifuatazo zinajitokeza: Ngoswe anapotoroka baada ya kumuiba Mazoea anasahau karatasi za takwimu ya hesabu ya watu kwa vile kitendo cha kumtorosha Mazoea kinamuudhi baba yake, baba huyo anaamua kuchoma moto karatasi za takwimu (uk 28)

Mapenzi ya ngoswe yanaonyesha kuwa ni ya kitoto, na kwavile ni ya kitoto, inaonekana wazi hayakufuata taratibu za mila na desturi zinazofuatwa na wanajamii.

Kutokana na hali hiyo, kazi ya kuhesabu watu inaharibika. Labda jambo la kusisitiza ni kuwa mapenzi ni kipengele tu kilichosaidia kuleta au kuharibu kazi.

Hasara za ulevi

Ngoswe – Penzi Kitovu cha Uzembe inaonyesha tatizo la ulevi linavyochanganya akila na kuharibu kazi nay a kuwa pombe inaathiri mambo mengi.

Ulevi unachelewesha kazi, Mfano wa wazi ni wakati wanapopanga kuanza kazi ya kuhesabu watu, kila wakiwafuata baadhi ya watu hukuta wamekwenda kwenye pombe. Mito mingi anasema (uk 6).

Mitomingi: Haya ni matatizo. Yote hii shauri ya pombe. Sina shaka yuko kilabuni.

Ngoswe: Haitasaidia. Mkewe tu hana habari ya kuhesabu watu, sembuse hao wengine! Kwa leo haiwezekaniki.

Pili Ngoswe na balozi Mitimingi walikunywa pombe aina ya mnazi mpaka wakalewa na kusababisha kuchoma baadhi ya karatasi za takwimu (uk 18-19) ulevi ni jambo la hatari katika kazi na ni lazima upigwe vita.

Umuhimu wa elimu

Elimu ni chombo muhimu kwa jamii kama inatumiwa inavyostahili. Katika tamthiliya hii, suala la elimu linaonekana kutotiliwa maanani sana na wanakijiji ambako Ngoswe alikwenda kuwahesabu. Familia nyingi zanaeleza kuwa watoto hawasomi kwa sababu shule ziko mbali na pale wanapoishi wao (uk16).

Kutokana na shule kuwa mbali yaelekea maendeleo ya kijiji yamebaki kuwa duni. Mfano unaoonekana ni ule wa huduma muhimu kama vile Hospitali kuwa mbali na pale wanapoishi (uk 16)

Ili kupata maendeleo suala la elimu lazima litiliwe mkazo, watu wengi wakielimika wataweza kutumia huduma vyema- kama vile kwenda hospitalini kwa matibabu kuliko kushiriki mitishamba tu.

Lakini kwa upande mwingine elimu imeonyesha kwenye tamthiliya hii kuwa ikitumiwa vibaya haiwezi kuleta faida. Kwa mfano Ngoswe aliyekuwa amepata elimu ya kutosha ameshindwa kuitumia vyema katika kuleta ufanisi wa kazi na kuleta amani na utulivu miongoni mwa wanajamii.g

Ili elimu iweze kuwa ya manufaa ni lazima itumike katika kuibadilisha jamii na kuisukuma mbele katika maendeleo. Na ili kupata maendeleo, lazima shule au huduma nyingine muhimu kama hospitali zisogezwe karibu na watu. Kijiji cha Mitomingi kinahitaji msukumo mkali ili kufikia maendeleo bora.

Malezi na ndoa za mitara

Kijiji kinachojadiliwa katika tamthilia hii kinaelekea kuwa katika mila na desturi za kuoa wake zaidi ya mmoja. Balozi Mitomingi ameoa wake wawili na kuna wanaume wengine waliofanya hivyo.

Suala la kuoa mitara limeonyesha athari mbovu katika malezi na utulivu wa familia nzima. Mwanaume akioa wanawake wengi familia inaongezeka na kuwa kubwa kiasi cha yeye kushindwa wakati mwingine kutoa huduma zinazotakiwa.

Familia ya Mitomingi ina watoto ambao huduma zao zinatia mashaka ndio maana pengine Mazoea aliweza kumkubalia Ngoswe ili kukimbia matatizo yanayojitokeza katika familia yao.

Pia wanawake walioolewa katika mitara hawaelekei kuwa na upendo wa kweli katika jamii yao. Kwa mfano, mama Inda na mama Mazoea hawakuwa wanapendana kwa dhati kwa wake zake wote wawili kwa kina kilekile. Kwa sababu ya kutopendana miongoni mwao ugonvi hauepukiki.

Ikiwa tabia ya kuoa wake wengi ni mila, basi hii ni mila isiyofaa. Sawa na hili pia, mila mbovu ambazo hazifai, kama vile kuchaguliwa mchumba kama ambavyo Mazoea alifanyiwa, sijambogg zuri. Tamthiliya ya Ngoswe inatoa tahadhari na hatari ya kuwa na mitara.

Hatari ya uvivu

Kijiji cha balozi Mitomingi kwa ujumla kinaelekea kuwa na watu wengi wavivu. Suala hili lauvivu linaelekea kuathiri kazi zozote zinazowahusu watu hao. Kutokana na uvivu, jamii ya Mitomingi haina maendeleo. Hakuna shule wala hospitali. Maisha yao ni ya ulevi tu. Watu wanajihusisha zaidi na ulevi kuliko kufanya kazi. (Hapa mwandishi anaitahadharisha jamii kuwa, uvivu ni sumu ya maendeleo).

Imani za uchawi na ushirikina

Jamii ya Balozi Mitomingi inaelekea pia kuwa na imani ya uchawi na ushirikina.

Kwa mfano, wakati wa kuhesabu watu baadhi wanaamini kuwa wachawi ndiyo wanaohesabu watu ili wawaue. (uk, 14),

Mama : “Sasa baba utatuhesabu vipi?”

Mitomingi: “Kwanini?”

Mama : Kama utatuhesabu wewe basi u mchawi”

Mitomingi: “Mbona sikuelewi!”

Mama : “Mchawi ndiye anayehesabu watoto wa wenzie ili awaroge sasa wewe umchawi? Hata
kama hu mchawi siwezi kukubali utuhesabu maana siwezi kujua kama nia yako
ni mbaya au nzuri.”

Kutokana na jamii ya Mitomingi kuwa na imani hii, zoezi zima la kuhesabu watu linakwama. Hali kadhalika katika jamii hii waliarnini kuwa mtu akifa basi amerogwa. Kama asemavyo mama wa kwanza. (uk. 16) “Wamemroga bure mume wangu. Alikufa akiwa na nguvu zake”.

Kwa ujumla haya ni mawazo ambayo hayana umuhimu wowote kwa jamii zetu. Kufa kwa mtu si kurogwa tu, ni pamoja na kutompeleka hospitalini. Hivyo msanii anatahadharisha jamii kuwa imani hizi potofu lazima zipigwe vita.

Nafasi ya mwanamke katika jamii

Tamthiliya ya Ngoswe imemchora   mwanamke katika vipengele   mbalimbali. Kwanza, kama chombo cha starehe. Katika kijiji hiki wanaume wanaonekana kuwatumia wanawake katika starehe. Hii inathibitishwa na tabia ya kuoa mitara kila mara ili wanawake watumike kukidhi haja ya wanaume.

Pili, amechorwa kama mzazi, Hapa wanawake wanaonekana wakijishughulisha na kazi za malezi baada ya kuzaa.

Tatu,   Amechorwa   kama   kiumbe. duni.   Hapa   mwanamke anadharauliwa   na mwanaume na akili zake kufananishwa na za mtoto. Mwanamke hathaminiwi na hafikiriwi   kuwa   anaweza kuchangia jambo   lolote la maana.   Wakati Mazoea

anatoroshwa na Ngoswe, Mitomingi anauliza (uk. 26),

Mitomingi: ‘ ‘Hivyo na nyie hamkuona dalili zozote juu ya watu hawa wawili?”

Mama Mazoea :   “Zilikuwepo “

Mitomingi       :           Kumbe mliziona mkanyamaza tu!”

Mamainda       :           “Sasa baba Mazoea tungefanya nini?”

Mitomingi:      :           “Mngefanya nini? Nyie wanawake akili zenu wote sawa.”  Si   Mazoea, si
mamayake….”                     

Kauli hii inaonyesha kuwa Mitomingi humthamini mke wake kwa sababu anaona kwamba hana akili za kikubwa. ni kama mtoto wake Mazoea, Tabia hii ya Mitomingi na ya wanaume wengi kuwadharau wanawake ni jambo ambalo lazima lipigwe vita.

Mvutano baina ya mji na vijiji

Mwandishi ameonyesha tofauti za kiutamaduni kati ya maisha ya mjini na yale ya vijijini. Tamthiliya hii inaonyesha athari za maisha ya mjini juu ya yale ya kijijini. Kwa mfano, utulivu wa kawaida wa kijijini tumeona jinsi unavyoingiliwa na fujo za mjini za akina Ngoswe.

Kitendo cha Ngoswe kumtorosha Mazoea bila ridhaa ya wazazi wake ni kinyume na taratibu za vijijini lakini ni jambo la kawaida kwa upande wa mjini na ni kutokana na kitendo hicho, Mitomingi anachoma karatasi za hesabu ya watu. Katika kutatua mvutano huo kati ya miji na vijiji Ngoswe anapendekeza kuwa,

“Hesabu ijayo ifikapo

Sharti vijiji kurekebishwa

Ujinga. Magonjwa na

Umaskini kupigwa vita

Na njia ni moja tu

Kuishi pamoja; kijamaa,” (uk. 29).

Wakati Ngoswe anapendekeza watu kuishi pamoja kijamaa kwa upande wa Mitomingi anaona kuwa kuna umuhimu vilevile kwa watu wa mjini kufundishwa kuishi kijamaa ili waweze kuyajua vizuri maisha ya watu wa kijijini na bila hivyo basi mvutano utaendelea kuwepo. Mitomingi anasema hivi,

“Mijini pia budi wafundishwe kuishi kijamaa maisha yetu kuyajua ama sivyo patatokea matata wawili hawa wakutanapo.” (uk. 30)

Kwa ujumla mwandishi anaona kuwa ili kuondoa mvutano huu kati ya miji na vijiji, ni lazima watu wa mjini wajifunze taratibu za maisha ya watu wa vijijini ambao bado hawajaathiriwa sana na utamaduni wa kigeni

Ujumbe

–       Si jambo zuri kuchanganya suala la kazi na starehe au mapenzi; wakati wa kazi uwe wa kazi na wakati wa starehe uwe wa starehe, na starehe ziwe mbali naofisi.

–       Wavulana wanaovuruga wasichana siku moja watakamatwa; na wasichana wenyewe wanapewa tahadhari kuwa wasifanye maamuzi bila kufikiri

–       Elimu ni kitu cha muhimu sana katika jamii na jamii isipokuwa na watu walioelimika haiwezi kuendelea.

–       Ili tuendelee tunahitaji kutupilia mbali ulevi na uvivu katika jamii zetu.

Migogoro

  1. Mgogoro kati ya Ngoswe na wazazi wa Mazoea, unatokana na uamuzi waNgoswe kumpenda Mazoea na kujaribu kumtorosha.
  2. Mgogoro kati ya Mazoea na wazazi wake unatokana na kitendo cha Mazoea kujaribu kutoroka na Ngoswe wakati anajua kuwa alikuwa anataka kuolewa.
  3. Mgogoro kati ya Ngoswe na serikali unatokana na kitendo cha Ngoswe kuharibu kazi ya hesabu ya watu,

edu.uptymez.com

Falsafa

Mwandishi anaamini kuwa jamii inaweza kuingia katika matatizo pale mapochanganya vitu viwili kwa wakati mmoja. Hivyo si vizuri Migogoro

kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.

Msimamo

Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi, kwani amezungumza wazi juu ya matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii kama vile umaskini, uvivu, ulevi. tatizo la ndoa za mitara na imani za uchawi na ushirikina.

Fani
Muundo

Muundo wa moja kwa moja umetumika. Tamthiliya imegawanywa katika maonyesho matano na kila onyesho lina kichwa cha kitaswira kinachoendana na yale yanayojadiliwa katika onyesho hilo.

Mtindo

Mwandishi ametumia mbinu ya dayolojia ambapo watu huzungumza wakijibizana na kutenda mambo mbalimbali, Katika kutajirisha mtindo wake, ametumia lugha ya kishairi pia (uk, 29 – 30).

Lugha

Tamthiliya ya Ngpswe Pen^i Kitow cha U^embe imetumia lugha laini (rahisi) na nyepesi inayoeleweka kirahisi. Licha ya hiyo ametumia tamathaU za semi na mbinu zingine za kisanaa. Pia kuna ujenzi wa taswira.

Misemo

–     Hebu keti tutupe mawe pangoni (uk. 11).

–     Kupeleka chakula ndio unafanya makao kabisa (uk. 1 1) .

Methali

Penye nia pana njia (uk. 22).

TamathaU za Semi

Tashibiha

–      Vumbi jekundu kama ugoro wa subiana (uk. 1).

–      Hebu kwanza tazama sarawili yake miguuni kama kengele ya bomani, (uk.    7).

–      Nilitoka hapa na kujitupa kitandani kama gogo. (uk. 18).

Tasfida

Wala hajarudi kama ingekuwa ni kujisaidia si angekuwa amekwishamaliza? (uk. 21).

Mbinu nyingine za kisanaa

mdokezo

–      Mazoea: Sijui … Siwezi… Narnuogopa baba (uk. 22),

–      Mltomingi:   Usizidl   kuniambia   mama;   Tambitambi   mambo   yake   hakuna
asiyeyafahamu … sasa mama …. (uk. 14).

Ngoswe: “Huyo mtoto wenu wa kwanza anaishi hapa au ….” (uk., 16).

Tunakaii Sauti

Mfano. Ngoswe anacheka. ha! ha!, n.k.

Takriri

–      Karibu. karibu (uk. 2).

–      Hodi! hodi! (uk. 5).

Taswira

Taswira mbalimbali zimetumiwa na mwandishi katika tamthiliya hii. Msanii ametumia taswira ya mto kwa kuhusisha na matukio ya wahusika. Mwandishi analinganisha mwanzo wa mchezo na kijito. kijito ni mto mdogo sana. Hivyo maelezo ya sehemu hii yanategemea kuwa madogo. Si makubwa. Matatizo yanayoelezwa katika sehemu hii ya awali tu.

Sehemu inayofuata inahusu vijito. Taswira ya vijito inaonyesha kuwa masuala yanayoshughulikiwa kujadiliwa hapa yanaongezeka ingawa bado si mazito.

Sehemu ya mto inaonyesha ukubwa wa shughuli ya Ngoswe. Ngoswe yuko kazini yuko mtoni tayari, yuko katika juhudi ya “kuvuka” kilichoko humo, bila shaka maji ya mto ni mengi (matatizo) na hivyo yeyote atakayeingia mtoni yampasa awe mwangalifu.

Sehemu ya jito inaashiria kuna hatari mno (matatizo). Kuna mengi katika jito. Kulivuka si kazi rahisi. Hatimaye tunaonyeshwa kuwa Ngoswe amezama baharini na amepotea. Tukihusisha na yale yaliyotokea na taswira ya bahari tunasema kuwa Ngoswe amezama, makaratasi ya takwimu yamechomwa moto na Mitomingi kutokana na kosa la kumtorosha Mazoea.

Wahusika

Ngoswe

Huyu ndiye mhusika mkuu katika tamthiliya hii. Ni msomi anayepewa kazi ya
kuhesabu watu. Lakini kutokana na tamaa ya mwili wake anaharibu kazi baada ya
takwimu zote kucttgmwa” moto na Mitomingi. Kutokana na kitendo chake cha
kujaribu kumtorosha ‘Mazoea bila ridhaa ya wazazi wake. Ngoswe ni mfano wa
watu wanaochangartya kazi na starehe. Matokeo yake ni kuharibu kazi. Hivyo hafai
Kuigwa.

Ngengemkeni Mitomingi

Huyu ni balozi na baba yake Mazoea. Ni mzee ambaye ameshikilia ukale na anayependa ndoa za mitara. Huyu anachoma karatasi za takwimu kutokana na Ngoswe kujaribu kumtorosha mtoto wake Mazoea.

Mazoea

Msichana mwenye umri kati ya miaka 18-20 ambaye ni mtoto wa balozi Mitomingi. Mazoea anawakilisha wanawake wasio na misimamo maalum katika mapenzi.

Mama Inda na Mama Mazoea

Hawa ni wake wa Mitomingi na walezi wa Mazoea.

Mandhari

Mandhari ya kijijini imetumika. Kijiji hicho kipo katika nchi ya Tanzania. (Aidha inawezakana kikawa kijiji chochote katika nchi zinazoendelea).

Jina la Kitabu

Jina la kitabu Ngoswe Penzi Kitovu cha uzembe linasadifu vizuri yale yaliyomo ndani ya kitabu hiki. Ngoswe ni jina la mhusika mkuu ambaye msanii anaonyesha jinsi kuendekeza kwake penzi kulivyomharibia kazi yake ya kuhesabu watu.

Kufaulu kwa Mwandishi

Mwandishi ameonyesha kwa Masi kikubwa kuyajadili matatizo yanayozikumba jamii zetu katika fani mbalimbali za maisha. Matatizo hayo ni kama uchawi. uzembe, n.k. Pia ametumia lugha rahisi inayoeleweka.

Share this post on: