Jina la kitabu: – Kilio Chetu
Waandishi – Medical Aid Foundation
Wachapishaji: TPH
Mwaka: 1996
Utangulizi:
Kilio Chetu ni tamthiliya iliyotungwa na Medical Aid Foundation. Katika tamihiliya hii kama asemavyo Vivian Mmari, Makamu Mwenyekiti wa Medical Aid Foundation katika utangulizi wake, Inajaribu kjvunja ukimya uliotawala miongoni mwa wanajamii katika kutatua matalizo makubwa ya kijamii yatokanayo na mahusiano ya kijinsia.
Tunasikia sauti ya jitimai itolewayo na watoto. Sauti iliyojaa sononeko na shutuma dhidi ya wazazi, walezi na watawaJa wenye kuufumbia macho msiba huu mkubwa wenye kuwaangamia.
Tunasikia sauti za vilio vya watoto wanaodai haki ya kuelimishwa kuhusiana na mambo yanayoweza kuathiri maisha yao. Wanataka wazazi, walezi na watawala wao kuwa wazi ill kunusuru maisha yao.
Hii ni tamthiliya inayopendekeza na kuibua mjadala miongoni mwa wanajamii kuhusiana na suala hili muhimu. Ni maoni ya mwandishi kwamba wakati tulionao sasa sio sawa na ule wa zamani. Mambo mengi yamebadilika, hivyo hata medani za vita hazina budi zibadilike katika kutatua matatizo ya wakati huu. Ushauri unaotolewa katika tamthiliya hii ni kwamba zile kuta zinazozuia mawasiliano ya wazi baina ya wazazi, walezi na watoto wao lazima ziangushwe.
Ni imani ya mwandishi wa tamthiliya hii kwamba, matatizo kama yale ya mimba katika umri mdogo, magonjwa ya zinaa kama UKIMWI, na kusambaratika kwa maadili katika jamii yanaweza kutatuliwa kwa kuwapa watoto elimu ya jinsia badala ya kuwajengea hofu na vitisho ambavyo kusema kweli vimedhihirika kuwa ni silaha duni katika mapambano haya.
Maudhui
TamthiJiya ya Kilio Chetu inabeba maudhui yanayozungukia mambo kadha wa kadha yahusuyo gonjwa hatari la UKIMWI, Kwa kutumia mbinu mbali mbali, mwandishi amelijadili kwa kina suala la malezi kwa \ijana/watoto. Anakemea vilivyo suala zima la mahusiano ya kijinsia wakati huu wa hatari tulionao. Pengine ni vizuri tukazipitia dhamira zilizojitokeza katika tamthiliya hii moja baada ya nyingine.
Dhamira
Dhamira kadhaa zimejitokeza katika tamthiliya hii na zinajionyesha wazi kupitia migogoro anayoijenga mwandishi na pia matendo ya wahusika.
Dhamira kuu
Elimu ya jinsia
Umuhimu wa elimu katika familia, hususani elimu ya jinsia ni suala ambalo limetawala katika tamthiliya hii. Kwa upande mmoja kuna wazazi/walezi ambao wapo teyari na wameamua kuvunja ukimya uliokuwepo kati yao na watoto wao na kuzungumza nao waziwazi juu ya masuala ya mahusiano ya kijinsia na hadhari zake. Wahusika hao ni mjomba na baba Anna. Mathalani baba Anna anasema:-
“Hili ndilo nimefaulu mwenzenu Nimemwambia mama Anna akae na mabinti nami nikae na wakiume …… Tumewaelimisha juu ya madhara ya tabia hiyo…“(uk. 10).
Kwa upande mwingine kuna wazazi/walezi wanaoshikilia ukale. Hawa bado wanaamini kwamba kutozungumza na watoto habari zinazohusu ngono kutawazuia wasijihusishe na mambo ya kujamiiana mapema. Mama Suzi na baba Joti ni watetezi wa msimamo huu. Matokeo ya msimamo huu ni kupoteza watoto. Kwa mfano, mama Suzi anasema:- “Tena ishia hapo hapo kaka! Huko si ndiko kunifundishia mwwanangu habari za ngono, ilitoka wapi hiyo?..”(uk.9).
Matokeo ya msimamo hii miwili imejadilliwa barabara katika tamthiliya hii. Mjadala unaohitimishwa kwamba ni bora watoto wakaelimishwa na kupewa habari sahihi kuhusiana na ngono na afya zao za uzazi kuliko kuwatia hofu na kuwatisha kwani hiyo kamwe haisaidii.
Mwandishi kwa kumtumia kumtumia Anna, binti ambaye wazazi wake wameamua kuvunja ukimya na kuongea naye waziwazi juu ya mambo ya mapenzi na hatari yake anatanabaisha faida za elimu hii. Anna mara zote anachukua uamuzi wa busara huku akijiamini kwa kila analolisema. Hii ni kutokana na msingi imara aliopewa na wazazi wake baada ya kuamua kuwa wazi kwake. Kuonensha namna Anna anavyopikwa akaiva kufuatia elimu ya jinsia aliyopewa na wazazi wake, mwandishi anamchora akisema:-
“Hujui, mjinga mkubwa we! Hujui kama kuna madhara mengine. Hujui magonjwa ya zinaa wewe, hujui kisonono, kaswende, na mengine kedekede, Haya hata juu ya UKIMWI hujui? Hebu nitolee uchafu wako mie ptuu!“(uk.25).
Kauli hii ya Anna inaonyesha jinsi ambavyo watoto, wawe wa kike au wa kiume, wakielimisha na wazazi, kwa vile ndio walimu wao wa kwanza, wanaweza kujijengea uwezo wa kujiamini na hivyo kuepukana na vishawishi vinavyoweza kusababisha maambukizo ya UKIMWI. Wanapotishwa bila kuambiwa ukweli wa mambo kwa visingizio vya makatazo ya dini, mila na desturi wanakuwa mbumbumbu katika suala zima la kujamiianana madhara yake ni kama tuonavyo kwa wahusika Joti na Suzi katika tamthiliya hii.
Dhamira ndogondogo
Zipo dhamira nyingine kadhaa ambazo zimejadiliwa chini ya dhamira kuu, nazo ni:-
Mapenzi katika umri mdogo
Kimsingi watoto wadogo (vijana wadogo) bawapaswi kujihusisha na mambo ya ngono mpaka hapo umri wao unapowaruhusu kuoa au kuolewa. Huu ndiyo msingi na msimamo wa mila na desturi za kiafrika na hata dini. Kinyume chake watoto wanaanza kushiriki vitendo vya kujamiiana katika umri mdogo jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao. Hiyo ndiyo hali halisi. Ni mara ngapi unasikia wanafunzi wa shule wanafukuzwa kwa sababu ya kubeba mimba? Hali hii imesawiriwa barabara katika tamthiliya hii ya Kilio Chetu. Watoto wa shule ya msingi kama vile Joti, Suzi na wengine wanaonekana kushiriki vitendo vya kujamiiana katika umri mdogo (uk. 16 -17, 19 – 21), Baya zaidi baadhi ya watoto wanashiriki matendo ya kujamiiana na wanawake au wanaume wanaowazidi umri., na pengine wenye wapenzi wengine jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao. Kwa mfano, katika tamthiliya hii, mwandishi anatanabaisha kuwa Joti alikuwa anaparamia mpaka wasichana wakubwa wa mitaaani. Kwa maneno yake mwandishi anasema:-
“Sasa ndiyo kuparamia mpaka wasichana wakubwa wa mtaani? Fikiri juu ya Chausiku, yule msichana mjuvi wa mji, ambaye pia anachukuliwa na yule Mpemba muu^a duka” (uk. 23).
Suala hili linaweza kuwa limechochewa pamoja na mambo mengine, kuzagaa kwa sinema za utupu, vijalida vanavyohamasisha ngono na zaidi ya yote, kuna mtandao wa internet ambao watoto wadogo wanatumia kuangalia picha za utupu zinazowahamasisha kufanya ngono. Mwandishi ameisawiri hali hii barabara. Anawaonesha vijana wanne, Joti, Jumbe, Choggo na Mwarami wakikumbushana kwenda kuangalia picha za -X, ingawa kuna zuio kwamba picha hizo ni kwa wakubwa tu (uk. 17-18).
Mapenzi na ndoa
Pamoja na kuwepo janga la UKIMWI bado watu wameendelea kutokuwa waaminifu katika ndoa zao. Wanandoa wanathubutu kutembea nje ya ndoa bila woga. Mwandishi anasawiri hali hii kwa kumtumia mama Joti. Mama Joti analalamika kuwa ndoa yake imeingiliwa. Hivyo kama suluhisho anaamua kununua kanga zenye maandishi yanayomsuta huyo anayeingilia ndoa yake. Mfano maneno
“Makapera kibao mume wangu wa nini” (uk. 7).
Swali la kujiuliza hapa ni je hili litasaidia? UKIMWI je? Mwandishi pia anafichua fikra za walio wengi kwamba wanaougua UKIMWI ni makapera na sio wanandoa (uk. 7). Hata hivyo dhana hii sio sahihi maana UKIMWI hauchagui wenye ndoa au wasio na ndoa.
Huduma kwa wenye Ukimwi
Mwandishi anajadili suala hili. Anatueleza kwamba.kugusana kwa kawaida na mgonjwa kugusa nguo zake na kupeana mikono na mgonjwa hakuambukizi mtu ugonjwa huo. Aidha anajadili umuhimk wa kumtunza mgonjwa wa UKIMWI. Ingawa hataji waziwazi, lakini anaongelea suala hili kwa kumtumia mhusika Mjomba (uk. 34). Mjomba anawashauri baba na mama Joti kumpa matunzo mazuri na upendo mgonjwa Joti. Anashauri mgonjwa asitengwe maana ugonjwa huu hauambukizwi kwa njia ya kuvuta hewa ya mgonjwa au kula naye. Zaidi mwandishi anasema;
“mgonjwa apewe chakula bora na yanapojitokeza magonjwa mengine kama malaria, apelekwe hospitali kwa tiba “(uk. 34)
na upendo mgonjwa Joti. Anashauri mgonjwa asitengwe maana ugonjwa huu hauambukizwi kwa njia ya kuvuta hewa ya mgonjwa au kula naye.Zaidi mwandishi anasema;
“mgonjwa apewe chakula bora na yanapojitokeza magonjwamengine kama malaria,apelekwe hospitali kwa tiba.”(uk.34).
Tiba ya Ukimwi
Kumekuwepo na mikanganyiko mingi miongoni mwa wagonjwa wa UKIMWI na jamaa wanaowauguza.Wengi wao hawataki kuamini kwamba wanaugua UKIMWI hata baada ya vipimo vya hospitali kuthibitisha hivyo.Badala yake hutawanya rasilimali zingewasaidia wao wakati wanaugua,na pengine familia zao baada ya kifo,katika kutafuta tiba za asili,Mwandishi akimtumia Mjomba analijadili jambo hili na kupinga waziwazi tabia ya kutapatapa anasisitiza tabia ya kuukubali ukweli ingawa unauma.
“……………ugonjwa huu hauna tiba.Ushahidi hupo wazi kabisa kwa kadri tunavyowaona wanaopata ugonjwa huu. Kwa hiyo si busara pia kuongeza matatizo hali ukweli tunaujua…“(uk.34).
Dhamira nyingine zilizojitokeza ni : athari zaakiw marafiki, Nafasi ya mwanamke katika jamii, Mila na desturi, n.k.
Nafasi ya mwanamke katika jamii
Waandishi wa tamthiliya hii ya kilio chetu wamemchora mwanamke katika nafasi na sura wa kadha wa kadha. Mathalani, wanamchora mwanamke akiwa mhuni na mwenye dhima ya kukidhi matamanio ya wanaume. Ni kwa kumtumia mhusika chausiku kwa mfano, waandishi wanatuonyesha namna mwanamke anvyotumiwa na mwanaume katika dhima hii. Chausiku licha ya kuwa mpenzi wa mpemba mwenye duka pia ni mpenzi wa Joti, kijana mdogo aliye bado mwanafunzi wa shule ya msingi. Mhusika mwingine mwenye kudhihirisha surah hii ya mwanamke ni suzi. Huyu ameumbwa katika sura ya kukidhi tama za mwili wa Joti.
Kadhalika, mwanamke anaonekana kuwa mnyonge na duni kiasi kwambahana uwezo wa kuchukua hatua zinazostahili anapoona ndoa yake imeingiliwa. Hili ni tatizo kubwa linalomkabili mwanamke hasa kwa wakati kama huu ambapo dunia imekumbwa na balaa la UKIMWI. Tunamuona mhusika Mama Joti angundua tatizo katika ndoa yake lakini honyeshi ujasiri wa kukaa na Baba joti na kulizungumzia suala hili la unyumba wao, nabadala yake anakimbilia kununua khanga ili kumsuta huyo “kidudu mtu” anyeisakama ndoa yake. Nafasi aliyonayo mwanamke katika asasi ya ndoa ndiyo haimruhusu wala kumpa mwanamke ujasiri wa kukaa na kuzungumza na mmewe kuhusu masuala haya.
Kwa upande wa pili wa shilingi, mwanamke katika tamthiliya hii anapewa nafasi kuwa mtu mhimu na wa kutegemewa katika malezi ya familia. Mathalani wahusika wanawake Mama suzi na Mama Joti wanaonekana kutoa mchango mkubwa katika malezi. Wako makini katika kufuatilia mienendo ya vijana wao na kuhakikisha kwamba wanakua katika misingi inayofaa. Tatizo pekee tunalohisi limechangia kwa wao kutofanikiwa katika ama yao ni njia walizotumiakatika malezi. Pengine wangeweza kufaulu kama wangetumia njia ya kuzungumza na kuwaelimisha watoto wao kama walivyofanya Baba na Mama Anna.
Aidha, mwanamke katika tamthiliyaa hji, imejengwa akiwa ni mwenye kuwa na msimamo Thabiti kama amejengewa msingi imara katika malezi yake, mwakilishi wa mwanamke kama kiumbe alien a msimamo madhubuti katika tamthiliya hii ni Anna. Anakataaa kufanya mapenzi katika umri mdogolicha ya kudanganywa kasha kutishwa na mhusika Mwarami. Ingawa ni wachache, lakini wapo wanawake wa aina ya Anna katika jami
Lakini pia, kupitia mhusika Anna, mwanamke anajitokeza kama mshauri na muelimishaji rika. Katika kutimiza Dhima hii, Anna anamshauri mwarami kwamba asikimbilie sut kabla ya kuvaa nepi. Maana yake ni kwamba hana budi kusubiri hadi hapo wakati utakapofika ndipo aingilie masuala ya mapenzi, na sio kufanya hivyo katika umri mdogo alionao.
Mila na desturi
Suala l mila na desturi zinazofungamana na ukale pia limechukua nafasi katika tamthiliya hii. Moja ya sababu zinazowafanya baadhi ya wahusika katika tamthiliya hii ya kutokubaliana na ushauri wa kuongea na watoto wao mambo yanayohusu kujamiana nipamoja na mila na desturi, Mila hizi, haziruhusu wazazi kuongelea masuala hayo na watoto wao wa kuwazaa.
Hata hivyo kushikilia mila na desturi hizi katika enzi hizi za UKIMWI ni sawa na kusema waache watoto afe kwa UKIMWI. Ni kutokana na athari jamii inazoweza kuzipata, waandishi wakasema pamoja na kwamba mila na desturi zetu haziruhusuwatu wazima, has wazazi, kujadili masuala wanayoyaita ya wakubwa na watoto wao wa kuwazaa, bado tunapaswa kuliangalia suala hili kwa jicho pevu. Pengine tuamue kuachana na mila na desturi hizo kwa lengo la kulinusuru taifa la kesho, Lazima jamii ikubali kuachana na maila ana desuri zilizopitw na wakati na kangalia njia ya kuwanusuruwatoto juu ya maambukizi ya UKIMWI.
Migogoro
Tamthiliya ya kilio chetuimejengwa juu ya migogoro kadhaa. Migogoro mingi ni kati ya kundi linaloshikilia ukale na lile linalotaka mabadiliko katika malezi ya watoto kuhusiana na elimu ya mahusiano ya kijinsia.
Mgogogoro wa kwanza ni kati ya mama suzi na bintiye. Mgogoro huu unatokana na vidonge vya kuzuia mimba kukutwa katika mfuko wa nguo za shule za suzi. (uk.7). mama suzi anchukua hatua ya kumwadhibu suzi kama mwarubaini wa kukomesha tabia hii bila kutmbua kwmba hofu na vitisho haviwezi kufua dafu mble ya silica ya mwili.
Mgogoro huu unaingiliwa na watu watatu. Baba Joti, ambaye anmuunga mkono mama suzi.Ili kusuruhisha mgogoro huu rai inatolewa kwamba lazima akina Mama Suzi wabadilike na wavunje ukimya uliotawala miongoni mwao kama kweli wamedhamilia kutatuamatatizo yanayoweza kuwaangamiza waoto wao.
Mgogoro mwingine ni kati ya Joti na mpenzie (Chausiku). Huu ni mgogoro unaotokana na tabia ya Joti kuwa na wasichana wengi anaotembea nao. Chausiku anamkaripia Joti kwa tabia hiyo chafu na anahahidi kumuunguza Joti na wasichana wake kwa moto hasa baada ya kugundua kwamba vitu anavyomhonga Joti anavitumia kwa wasichana wake wengine (uk. 22). Chausiku anasema:-
“me nakununulia fulana ya mazoezi wewe unahonga kinyago chako kile…… Nikikupa hela ya kununua peni we unanunulia bazoka visichana vyako”
Pia kuna mgogoro kati ya Mwaratni na rafikize ( Joti na Jumbe) juu ya suala la ngono, Mwarami na Anna juu ya suala la kufanya ngono katika umri mdogo, Suzi na Anna juu ya suala la utoaji mimba nk.
Ujumbe na Maadili
Baada ya kuisoma tamthiliya hii tunapata rundisho kuwa kweli “Asiyefunzwa na wazazi hufunzwa na Ulimwengu” ikiwa na maana kuwa mafunzo wayapatayo watoto toka kwa walezi wao ni bora na ndiyo yawasaidiayo kuishi kwa kujiamini na kutohadaika na mambo yasiyofaa. Hivyo si vizuri kuwanyima fursa hiyo kwa kisingizio cha dini, mila, desturi au sababu nyingine yoyote.
Mwandishi anatoa ujumbe kwamba ugonjwa wa UKIMWI hauenezwi kwa njia za kugusana au kula na mgonjwa. (uk. 34) bali ni kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye ugonjwa huo. Ujumbe huu unasawiri mazingira yetu kwa sasa ambapo kuna ongezeko kubwa la maambukizo ya ugonjwa wa UKIMWI. Hivyo anatoa wito kwa wazazi na walezi kutofumbia macho hali hii bali wawe wazi kwa watoto wao kwa kuwapa elimu ya kijinsia na jinsi ya kuepuka ugojwa huu. Kwani hauna kinga wala tiba.
Mtazamo na msimamo wa mwandishi
Msanii anautazama ulimwengu kwa jicho pevu na yakinifu. Anauona kama kitu kinachobadilika, hivyo hata jamii inapaswa kubadilika. Anayachunguza mazingira yanayo mzunguka mtoto katika zama hizi na kugundua kwamba watoto wako hatarini kuteketea kutokana na kukosa habari zozote za kuwasaidia. Mwandishi anatoa msimamo ambao ni tofauti na wazazi/walezi wengi. Msimamo wa kuvunja ukimya na kuzungumza na watoto kwa kuwapa elimu ya jinsia ili kuwanusuru wasiangamie.
Falsafa ya Mwandishi
Mwandishi anaamini kwamba kuwapa watoto elimu ya familia ikiwa ni pamoja na elimu ya jinsia si kuwafundisha umalaya kama wanavyoeleza wapinzani wa hoja hii. Badala yake, ni kuwafanya watoto wajitambue na kuyaelewa barabara madhara ya kujiingiza katika matendo ya kujaamiiana katika umri mdogo, Hii ndiyo njia pekee ya kuwanusuru vijana/watoto dhidi ya “dubwana” linalotishia maisha yao. Hii ndiyo falsafa ya mwandishi wa tamthiliya hii.
FANI
Tamthiliya ya Kilio Chetuimedhihirika kuwa ni mojawapo ya tamthiliya zenye utajiri wa vipengele vya kifani. Mwandishi amtumia vipengele kadha wa kadha vya fani.
Katika kufikisha maudhui yake kwa walengwa. Vipengele vya fani ambavyo vimejitokeza mara kwa mara katika kazi hii ni hivi vifuatavyo:
Wahusika
Wahusika wa fasihi ni watu ama viumbe wanaowakilisha tabia halisi za watu katika jamii. Tamthiliya ya Kilio Chetu ina jumla ya wahusika kumi na wawili, na wengi wao karibu wana hadhi sawa kiasi kwamba sii rahisi kuwatenga katika makundi ya wahusika wakuu na wadogo kama tulivyozoea.
Wasifu wa Wahusika
Mama Suzi:
Huyu ni mama yake Suzi. Ni mwenye kushikilia msimamo wa kizamani, kwamba mzazi hawczi kuongea na mwanae masuala ya kujamiiana (uk. 6). Haamini kwamba watoto wadogo, kwa mfano, wanaosoma darasa la tano wanaweza kuwa wameanza tabia ya kujamiiana (uk. 5). Kwa maneno yake anasema:
“Fausta alikuwa mtoto sana. Mtoto wa darasa la tano. Mambo hayo asingeyajua” (uk. 8.)
Mama Suzi anawiakilisha kundi la wazazi ambao hawaamini katika kusema na watoto wao mambo yanayoweza kuhatarisha maisha yao, kwa mfano, anapomkuta mwanae Suzi ana vidonge vya kuzuia mimba anachukua jukumu la kumpiga badala ya kumwelimisha juu ya madhara yake (uk. 7 – 9). Haamini kwamba binti mdogo kama Suzi anaweza kuyafahamu mambo ya kujamiiana mpaka anapomkamata na vidonge vya kuzuia mimba. Ndipo anasema:
“Mwanetu huyu keshakua sasa anabugia vidonge vya kuzuia mimba … wewe unataka kuniumbua mie, we mbwa mweusi… ” (uk. 8).
Suzi
Huyu ni mtoto wa mama Suzi. Ni binti mdogo anayesorna darasa la sita. Ni mpenzi wa Joti, mwanafunzi mwenzake. Amekwisha jiingiza katika masuala ya mapenzi katika umri huu mdogo kinyume na matarajio ya mama yake. Mwanzoni mama yake hakuwa na habari kuhusiana na tabia hii ya Suzi hadi alipomkamata na vidonge vya kuzuia mimba (uk. 8). Anamwogopa mama yake sana lakini hawezi kushinda nafsi yake iliyokwishatekwa na mambo ya ngono kutokana na ukosefu wa elimu juu ya mambo haya. Anapata mimba na inaelekea ana UKIMWI kwani Joti aliyempa mimba hiyo imedhihirika kuwa ana UKIMWI.
Baba Joti
Huyu ni baba yake Joti kijana ambaye amepata ugonjwa wa UKIMWI kutokana na kijiingiza katika mambo ya mapenzi akiwa mwenye umri mdogo. Ni jirani yake na akina Mama Suzi. Kama alivyo Mama Suzi, Baba Joti pia haamini katika kuwaelimisha watoto kuhusiana na masuala ya kujamiiana. Anamwona Suzi kuwa ni “kitoto kidogo” kama alivyo mwanae Joti hivyo kumpa elimu ili aifahamu jinsia yake na ajijue alivyo ni kumharibu.
Sado ameshikilia msimamo wa kizamani kwamba wazazi hawawezi kukalishana kitako na watoto wao na kuwaeleza habari za ngono (uk.10). Kwa mawazo yake,dawa peke ya kuwadhibiti watoto wasijiingize katika masuala hayo ni viboko au mijeledi tu (uk. 10).
Mama Joti
Huyu ni mke wa Baba Joti na mama yake Joti. Anaamini kuwa watoto wanajua makubwa maana “Wembamba wa reli treni inapita” (uk. 6). Hakubaliani na kitendo cha kumkingia kifua mtoto maana si rahisi kujua huko waendako wanafanya nini (uk. 6). Ndoa yake imo matatani kufuatia kuingiliwa na nyumba ndogo yeye anaita “Kidudu mtu” (uk. 7).
Mjomba
Ni kaka yake Mama Suzi. Ana upeo rnpana wa kuelewa mambo. Anafahamu ulimwengu wa sasa ulivyo. Maoni yake ni kwamba watoto wapewe elimu ya familia, ikiwa ni pamoja na elimu ya jinsia ili waweze kujua kinagaubaga juu ya mambo yahusuyo mapenzi na hatma yake. Anamini kwamba hii itasaidia kuwaonesha watoto madhara ya kufanya mapenzi kabla ya ndoa. Ana ushauri mzuri, anamshauri Baba Joti asihangaike kwenda kwa waganga wa jadi kwa ajili ya tiba ya Joti aliyegundulika kuwa ana UKIMWI. Badala yake anashauri Joti apewe matunzo mazuri ili aweze kuishi kwa matumaini (uk. 34).
Baba Anna
Kama mjomba, Baba Anna pia ana upeo mpana wa kuelewa mambo. Yeye na mkewe, mama Anna, wameweza kukaa na watoto wao na kuwaelimisha juu ya madhara ya tabia ya kufanya mapenzi katika umri mdogo. Kwanza kwa watoto wenyewe na pia kwa familia nzima na hasa kwa wazazi wao (uk. 10). Anaamini kwamba iwapo watoto wataelimishwa barabara kamwe hawatathubutu kujihusisha na masuala ya kujamiiana.
Jirani
Ni jirani yake Baba Joti. Hana imani na matokeo ya vipimo vya hospitali hivyo anashauri wampeleke Joti kwa “mafundi” zaidi wa tiba. Huyu anawakilisha wananchi wengi ambao hawataki kuamini kwamba UKIMWI upo katika jamii, na mtu ukimpata sio kwamba amerogwa.
Chauslku
Ni msichana wa mtaani, jirani na akina Suzi. Si msichana mzuri kitabia. Anafanya mapenzi na watoto anaowazidi mbali kwa umri. Ni mjuvi wa mji na anachukuliwa pia na Mpemba mwenye duka.
Chogo, Mwarami na Jumbe
Wavulana wanaosoma pamoja na Joti. Kama Joti, nao wamekwishajiingiza katika mapenzi na wasichana. Wana tabla ya kuangalia magazeti ya picha za uchi na sinema za “X”. Wana tabia ya kukaa vijiweni na mazungurnzo yao ni kuhusu masual,.a ya ngono.
Joti
Mwanafunzi wa shule ya msingi darasa moja na akina Suzi, Chogo Jumbe na Mwarami. Ana mahusiano ya kimapenzi na wasichana kibao, kwa mfano Suzi, Chausiku, Yoranda, Gelda na Sikujua. Kwa sababu wazazi wake hawakuongea naye ili kumpa elimu juu ya athari za ngono aliendelea na tabia hii hadi akaukwaa UKIMWI
Muundo:
Tamthiliya ya kilio chetu imechuka muundo wa moja kwa moja, yaani sago. Visa vinaelezwa kwa mtiririko bila kukatizwa. Mchezo unaanzia katika sehemu ya kwanza ambapo maelezo kuhusu kuingia na dubwana (UKIMWI) katika kisiwa kunaelezwa. Sehemu ya pili intujulisha juu ya kifo cha Fausta na pia habari za Suzi kufanya mapenzi zinajulikana kufuatia kukutwa na vidonge vys kuzuia mimba katika mfuko wake. Ni katika sehemu hii mjomba na baba Anna wanaelezea umhimu wa elimu ya jinsia ili kuwanusuru watoto na janga hili la UKIMWI.
Ni katika sehemu ya tatu na ya nne inpodhihirika kwamba wanaoitwa watoto si watoto tene maana wameshajiingiza katika mambo ya ngono, na hivyo wako hatarini kuangamia. Mahusianao ya kati ya joti na Suzi, na wasichana wengine kama vile Chausiku, Yoranda, Gelda na Sikujua yamefunuliwa katika sehemu hizi. Aidha, kwa kututmia mhusika Anna, inaoneshwa katika sehemu ya nne, namna motto aliyepwa elimu ya jinsia anavyoweza kukabiliana na vishawishsi na hivyo kuepukana na balaa la UKIMWI
Sehemu ya tano, suzi anagundulika kuwa na mimba ya Joti . sehemu ys saba intupeleka nyumbani kwao Joti ambapo inadhihirika kwamba joti anaugua UKIMWI na ushsuri unatolewa na mjomba kwamba apewe matunzo mazuri ili aweze kuishi kwa matumaini.
Mtindo:
Mwandishi wa tamthiliya hii amedhamilia kuifanya tamthiliya yake iwe na umbo la kiafrika kufuatia kutumia baadhi ya vipengle vya sanaa za maonyesho za kiafrika katika tamthiliya hii ya kilio chetu. Baadhi ya vipengele hivyo ni pamoja na matumizi ya nyimbo, (uk.1)……, niendelee, nisiendelee?……au mmechoka? (uk.113). pia katika uk. 36, mwandishi anamalizia …Na hadithi yangu imeishia hapo.
Mwandishi pia amemtumia mtambaji kutoa maelezo na ufafanuzi kuhusu matndo ya wahusika na matukio katika tamhiliya yake , mtindo uliozoeleka.
Aidha, mwandishi ametumia mtindo wa diologia. Amefaulu kuleta diologia inayovutia na kuaminika baina ya wahusika.ni diologia ambayo, kwa kweli, ametumia maneno machache lakini yaliyoteuliwa kwa ufundi na ustadi mkubwa sana.
Matumizi ya lugha:
Mwandishi wa tamthiliya hii ya kilio chetu ameonesha ustadi mkubwa katika uteuzi wa lugha ya kutumia. Ametumia lugha inyowafanya wasomi watafakari kwa.
Makini kile wanachokisoma, Lugha iliyotumika ni nyepesi kwa hadhira lengwa, yaani watuwa kawaida, hasa wazazi la walezi. Aidha ni lugha iliyoshehenezwa tamathali za semi na mbinu nyingine za kisanaa
Methali,
“Asiyefundwa na mamaye hufundwa na walimwengu” (uk.36)
“Wembamba wa reli treni inapita “(uk. 6)
Misemo;
“….kukimbilia suti na nepi hujavaa” (uk.26)
“Mapenzi ni tiba” (uk. 22)
: Nakuwa nyumanyuma Kama koti” (uk.4)
Útakatifu wa usoni” (uk.4)
Nahau
“kufa kwa kunyaga nyaya” (uk.4)
Matumizia ya lugha ya kingereza na asili
Mwandishi ingawa ni Kwa kiasi kdogo, ametumia lugha ya kuchang’nya lugha ya Kiswahili na kingereza. Lengo hasa la kuchanga’nya lugha lilikuwa ni kusawiri namna nijana weing wa siku hizi wananyoongea Kwa kuchanga’nya Kiswahili na kingereza. Mfano mzuri 9uk.16)
“Ndo ume-come sio?”
Kwa upande wake, lugha ya asili haijatumika katika mazungumzo ya kawaida. Imetumika tu katika wimbo wa maombolezo (uk.35)
Tamathali za semi.
“Mbona unakuwa mgumu Kama mpingo”? (uk.5)
“Miti inayoungua Kama mabua” (uk.6)
“…..Wakapukutika Kama majani” (UK 3)
Sitiari
“Ndio wa kumvumilia buyu nguru anayechimba ndoa yangu” (uk.7)
“Huyu kinyago wako anakimbia nini?” (uk. 21)
Mbinu nyingine za kisanaa
Onamatopea
“Wacha moyo unipwite pwi, pwi, pwi,” (uk .16)
“Basi vupu nikadondoka….” (uk. 16).
Takriri;
“Piga domo, piga domo” (uk.16).
“Watu walipukutika, wakapukutika Kama majani ya kiangazi; wakapukutika” (uk.1).
UJENZI WA TASWIRA
Mwandishi anatujengea taswira ya Dubwana lililoleta balaa kisiwani (uk. 1).
Anaeleza kwamba kila mtu aliyeguswa na dubwana hili alipata madhara. Watu waliotoka mapele, wakaharisha, wakanyonyoka nywele, wakakonda na kupoteza uzito kabla ya kufa. Haya ni maelezo yanayomfanya msomaji ajenge woga juu ya dubwana hili yaani UKIMWI.
Mandhari
Mandhari katika tamthilia ni ile sehemu au mazingira ambamo makutano yanatokea. Mandhari ya tamthilia hii ni ya mjini. Hii inathibitishwa na mhusika jirani anaposema:
“Mie toka siku ile niwaone hospitali sijakaa mjini. Nilikwenda zangu shamba kupambana na nyani wala nafaka” (uk.32)
Lakini pia habari za kuangalia sinema za “X” (uk.18) zinatuthibitishia mandhari ya mahali matendo haya yanapotendeka ni ya mjini. Zaidi ya hapo, lugha inayozungumzwa na wahusika vijana kama vile Joti, Jumbe, Chogo na Mwarami ni lugha ambayo imezoeleka mazingira ya mjini kulIko vijijini (Rejea kwa mfano mazungumzo yao (uk.16).
Tunaelezwa pia kwenye tamthilia hii kwamba mhusika Mwarami alikuwa akimnunulia Anna soda na mihogo kule uwanja wa Sabasaba (uk.26). Zaidi Anna anaeleza katika wimbo wake kuwa hataki pesa za wanaomhonga wala lift zao (uk.27). Ni wazi kwamba uwanja wa Sabasaba upo mjini na lift kwa akina dada, hasa wanafunzi zinatolewa mjini kuliko vijijini.
Jina la kitabu
Kilio chetuni jina la kitabu linalo akisi yale yaliyo katika kurasa za ndanio zatamthiliya hii.Kilio chetuni kilio cha jamii nzima kuhusu gonjwa la UKIMWI. UKIMWI umepoteza maisha ya watoto, vijana, wazazi na ndugu zetu ambao ni muhimu sana kwa ustawi wa familia na jamii kwa ujumla.
Kilio chetu kama jamii ni muhimu ili kuonesha huzuni yetu dhidi ya gonjwa hili la UKIMWI ili jamii isiendelee kuwa na kilio.
Kwa ujumal, kilio chetu ni jina la kitabu ambalo lina sadifu yaliyo ndani kwa namna mbili.
- “Kilio chetu” ni kielelezo cha huzuni walizonazo wahusika ndani ya kitabu kutokana na ugonjwa wa UKIMWI kuathiri watu wengi.
- “Kilio chetu” pia inawakilisha mahitaji au matakwa ya kuwepo kwa elimu ya UKIMWI na Jinsia ili kupambana na UKUIMWI.
edu.uptymez.com
Hivyo, Kilio chetu imesadifu yaliyomo ndani ya kitabu kwa kuonesha vilio vinavyotokana na UKIMWI na pia vilio vya kuhitaji msaada madhara ya UKIMWI.
KUFAULU N A KUTOFAULU KWA MWANDISHI
- Kufaulu
edu.uptymez.com
Kimudhui, mwandishi amefaulu kueleza jamii UKIMWI ni kitu gani, njia zinazoambukiza na kujikinga na namna ya kuhudumia wagonjwa wa UKIMWI. Mwandishiamesisitiza umuhimu wa Elimu, uwazi na ukweli kama mbinu muhimu ili kuvunja ukimva.
Kifani, mwandishi ameweza kuumba wahusika wa rika tofauti amabao ni muhimu katika kupambana na UKIMWI
B. Kutofaulu
Mwandishi ameonesha vijana ndio waathirika pekee wa UKIMWI. Mwandishi angeweza kwenda mbali zaidi kuwa watu wazima, na hata baadhi ya watu wanonesha kama watakatifu wanaweza kuwa chanzo cha UKIMWI. Mwandishi angeweza kugusa hata ndoa. Namna watu wanavyopaswa kulinda na kuheshimu ndoa zao ili kuepuka UKIMWI. Mama wajawazito wangehimizwa zaidi kupima virusi ili kuwa namna ya kumsaidia kiumbe aliye tumboni. Si wote wenye UKIMWI hupata kwa njia ya ngono, kuna wengine hupata virusi vya UKIMWI kwa njia nyingine.