Form 4 Kiswahili – VITABU TEULE VYA FASIHI

Share this post on:

                                               RIWAYA

RIWAYA:   WATOTO WA MAMA NTILIE

MWANDISHI:   EMMANUEL MBOGO

Utangulizi :

Watoto wa mama Ntilie ni riwaya iliyotungwa na mwandishi maarufu wa riwaya na tamthilia Emmanuel Mbogo na kuchapishwa na Heko Publishers Ltd Mwaka 2002. Ni riwaya inayochambua kwa kina adha wazipatazo watoto wa mama ntilie. Hawa wametapakaa mjini huku wakifanya biashara ya kuuza vyakula ili kutafuta chochote cha kuwawezesha kutunza familia zao.

Mwandishi hapa anatueleza kuwa wakina mama hawa wanaishi maisha magumu. Watoto wao ambao wangewasaidia hapo mbeleni hawapati elimu kutokana na kukosa mahitaji muhimu ya shule, matokeo yake wanajiingiza katika matendo maovu ikiwa ni pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya, uvutaji bangi na ujambazi.

MAUDHUI
Mama ntilie: Ni riwaya ambayo imesheheni maudhui ambayo kimsingi yanazungukia maisha ya mama ntilie na familia zao kama sehemu ya walala hoi waishio katika miji na vitongoji mbalimbali hapa nchini. Katika riwaya hii mwandishi amejadili dhamira mbalimbali na kutoa ujumbe mzito katika jamii na dhamira hizo ni kama zifuatazo.

DHAMIRA
Dhamira zilizojitokeza katika Riwaya hii ni kama vile suala la umaskini, elimu, mapenzi, malezi, ujambazi, nafasi ya mwanamke, ulevi wa pombe n.k.
Dhamira zilizojitokeza katika riwaya hii ni kati ya hizi zifuatazo:

  1. UMASKINI

edu.uptymez.com

Hili ni suala ambalo limeongelewa kwa kiasi kikubwa katika Riwaya hii, takribani wahusika wote waliozungumzaiwa katika riwaya hii ni maskini.   Tukiwaangalia Mama ntilie na familia yake tunaona kwamba katika familia hii maisha hayawezi kwenda bila mama ntilie kwenda kwenye biashara zake za kupika chakula. Katika genge lake la Urafiki (UK.14) kilichopatikana kuishia tumboni.

Ni Umaskini huu pia uliwakabili Dotto na Kurwa watoto mapacha walioachwa yatima baada ya wazazi na walezi wao kufariki (UK54). Ni hali hii ya Umaskini iliyowakabili Dotto na Dani kwa kufanya wizi ambao uliwagharimu maisha yao yote (UK.43-47)

Pamoja na mipango mizuri ya serikali katika kuondoa umaskini. Mbogo anatueleza kwamba hakuna jipya bado watu wanaishi katika lindi la Umaskinini ambayo ilidhirishwa na wahusika Kurwa, Dotto, Peter na watu wengine wengi wakubwa kwa watoto wanaopigana vikumbo kule dampo.(UK.26). Mwandishi anasema:
” watu waliosongamana! Kupigania mchele, wengine walikuwa na vikapu, wengine magunia.

  1. SUALA LA ELIMU

edu.uptymez.com

Elimu ni kitu muhimu kwa watoto kama taifa linataka kuendelea hapa watoto kutoka familia maskini bado hawana uhakika wa kupata elimu licha ya porojo mwandishi anawasaili watoto wa shule ya msingi Makurumla na mwalimu wao mkuu Chikoya. Mwandishi anasema:
“Wote ambao hamna ada na sare hakuna shule! Nisizione sura zenu bila ada na sare. Waambie wazazi wenu hivyo” (UK.1)

Hapa tunaona kuwa kumfukuza mtoto shule eti kosa hana Ada au Sare ya shule ni kunyima mtoto haki yake ya msingi ya kusoma.
Mwandishi anatueleza kuwa Peter alipenda sana shule, pamoja na kufukuzwa shule alijitahidi kutafuta Ada na Sare za shule ilikuweza kurudi shuleni (UK.9) hata hivyo ndoto yake haikutimia umaskini ulimkaba mpaka akashindwa kufurukuta.

  1. SUALA LA MALEZI

edu.uptymez.com

Riwaya hii imejadili suala hili kwa kina kwa kutumia wahusika Musa, Dani, Dotto na Kurwa, Peter na Zita. Hapa mwandishi anaonyesha umuhimu wa kuwa wazazi wote wawili. Musa katika Riwaya hii hana baba (UK,17) amelelewa na mama tu hali kadhalika Dani (UK38). Hali ni mbaya zaidi kwa Doto na kurwa kwani hawana wazazi wala walezi mambo ni tofauti kwa watoto wa mama ntilie Zita na Peter pamoja na maisha Duni wanayoishi lakini hawakujiingiza katika uovu.

  1. NAFASI YA MWANAMKE KATIKA JAMII

edu.uptymez.com

Mwandishi wa kitabu cha Watoto wa mama ntilie amechora mwanamke kama ni mhimili wa kiuchumi na kijamii katika familia. Mfano ni mama Zita na Peter alikuwa akiuza chakula na kuweza kuwahudumia watoto wake.

Kwa wale wanawake walioajiriwa katika kazi za kijungujiko na pengine zinazowadhalilisha kama vile uuzaji baa, kazi anayoifanya Zenabu (UK5.na 29). Ni ukweli usiopingika kwamba asilimia kubwa ya wafanyakazi wa baa ni wanawake.

Hapa wanawake wamesawiriwa kama watu wenye huruma na roho ya kupenda kutoa msaada.

Wanawake watatu wametumiwa na mwandishi kujadili suala hili kama Jane, rafiki yake Mama Kurwa huyu aliwahurumia watoto wa marehemu na aliwatunza hadi kifo chake(UK37)
Mwingine ni Kurwa aliyemhurumia Peter wakati Doto amempiga na mwenye huruma ni Zenabu.

  1. ULEVI

edu.uptymez.com

Dhamira hii pia imejitokeza katika riwaya hii ya watoto wa mama ntilie. Mwandishi anelezea habari za mzee Lomolomo, mlevi wa chang’aa mataputapu na gongo (UK10,70,71,72) hapa kwa kutumia mzee Lomolomo, Emmanuel Mbogo anaisawiri  barabara jamii ya Tanzania kuwa badala ya kuthamini familia na kazi wao wanaendekezeka pombe.

  1. WIZI, UJAMBAZI NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

edu.uptymez.com

Hapa mwandishi anelezea jinsi wizi, ujambazi na biashara ya madawa ya kulevya ilivyo haribu watoto, vijana wengi wamechora kwa kukimbilia vitendo hivi vichafu kama suluhisho la umaskini unaowakabili: Mfano Dani kwa kukosa malezi anaamua kujiingiza katika wizi (UK.38) mwingine ni Doto na dada yake Kurwa. Walifanya mpango na kwenda kuvamia duka la Rhemtula (UK40-43).

Wahusika wengine waliojihusisha na mambo ya wizi na ujambazi ni Dotto pamoja na Kurwa

Matokeo ya ujambazi huo yalipelekea kuuwawa kwa Dani na Dotto (UK.45) Mwandishi anatuelezea namna walivyouwawa:

“Paa! Paa! Bastola ililia, Mlinzi Simango alifyatua bastola. Kivuli cha juu kilitoa ukulele wa uchungu “Aaa!” kikadondoka   chini.”

“Kivuli cha chini hakikuzubaa, kilitumia mbio kama swala, chaa!

“Wapi! Simango alilenga Paa! Paa! Paa! Mara tatu Kurwa alisikia tena sauti ya uchungu “Aaa!”(UK.45)

  1. MAPENZI

edu.uptymez.com

Mhusika Peter ndie anayeiwakilisha dhamira ya mapenzi ya kweli dhidi ya binti Kurwa. Hapa pamoja na misukosuko aliyoipata Peter toka kwa dada yake (Zita) Piter hakusita kuonyesha dhamira yake ya kusaidia kurwa.

“Tungoje mama arudi, lakini siwezi—— hatuwezi kumfukuza, tukamwacha ateseke tu huko mitaani(UK.65)

MIGOGORO

Migogoro kadhaa imejidhihirisha katika Riwaya hii hivyo si mingi sana ikilinganishwa na kazi nyingine za mwandishi kama vile Tone la Mwisho ngoma ya ng’wanamalundi, Giza limeingia ambazo ni tamdhilia. Migororo takribani yote ni ya akina Siye, wao kwa wao.

Mfano kuna mgogoro kati ya Doto na Peter

Mgogoro kati ya Zita na Kurwa.

Mwandishi pia amefaulu kujenga mgogoro wa nafsi Kurwa anachora akiwa na mgogoro wa nafsi, Anawaza juu ya maisha yake na namna alivyokosa mapenzi ya wazazi baada ya kuwaona watoto wawili wakipita na mama yao.

MAFUNZO NA MAADILI

Mwandishi wa watoto wa mama ntilie ni mwalimu na mwandishi wa jamii.

Kwanza : tunapata ujumbe kwamba uhalifu haulipi mema, ndivyo ilivyo tokea kwa wahusika Dani, Doto, Musa na Peter.

–         Wakati Dani na Doto wanapoteza maisha, Musa na peter wanaishia jela.

Pili : tunapata ujumbe kwamba si vizuri kuwafukuza watoto shule eti kwa sababu ya kukosa Karo au Sare maana wao hawaba hatia katika hilo.

Tatu: Akina mama ntilie wana kazi nzito ya kulea taifa la kesho, hivyo jamii lazima iwasaidie katika kuubeba mzigo huo.

Nne: Pia ujumbe mwingine ni kwamba ulevi si kitu kizuri mf. Mzee Lomolomo.

Tano : Mwisho watoto yatima wanahitaji msaada katika jamii.


FANI

Wahusika wa riwaya ya watoto wa mama ntilie wanaweza kugawanywa katika makundi mawili ya wahusuka wakuu a wasaidizi. Wahusika wa kuu wanajitokeza tanngu mwanzo mwa hadidhi hadi mwisho.

WAHUSIKA:

Mama ntilie (mama Zita)

Huyu ni mke wa mzee Lomolomo

Mzee Lomolomo

Mumewe mama ntilie na baba yao Zita na Peter

Peter

Ni mototo wa kiume wa mama ntilie

Zita

Ni mototo mwiingine wa mzee Lomolomo na mama ntilie

Mwalimu chikoya

Ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi makurumla

Doto na Kurwa

Hawa ni watoto mapacha hawakumjua baba yao

Zenabu

Msichana rafiki na jirani wa mama ntilie

Musa

Ni mmoja wa wanfunzi waliofukuzwa makurumla

MUUNDO

Visa katika riwaya ya watoto wa mama ntilie vinaelezwa kwa namna ya kurukiana

MTINDO

Mwandishi ametumia zaidi nafsi ya tatu, umoja na wingi. Huu ni mtindo wa kawaida na uliozoeleka. Aidha kuna matumizi ya nafsi ya kwanza nay a pili katika vipengele vichache tu vinavyotumia dialogia.

Aidha mwandishi ametumia mtindo wa kifasihi simulizi, mtindo ambao unajitokeza katika matumizi ya nyimbo mbalimbali.

MATUMIZI YA LUGHA

Riwaya ya mama ntilie imeandikewa katika luhga ya moja kwa moja na inayoeleweka kwa walengwa

MANDHARI

Watoto wa mama ntilie ina mandhari ya jiji la Dar es salaam. Mitaa ya jiji mfano kisutu kiwanda cha Urafiki, Manzese, shule ya msingi Makurumla, dampo la Tabata n.k. Ni kwamba kwa wasomaji walio kwishafika jijini Dar es salaam watakuwa wanapata picha ya maeneo hayo.

Share this post on: